Thursday, July 2, 2015
Nkupamah blog
Staa mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee
Majuto’ amefungukia shutuma anazopewa na mashabiki wake kwa kupenda
kuonekana na ‘vibinti’ kuwa wanamshobokea mwenyewe.
Mzee Majuto ambaye kifani ni bingwa wa
komedi amesema, kutokana na kazi yake ya uigizaji imemfanya kuzimikiwa
haswa na mabinti.
“Sijawahi kumshobokea binti yoyote ila wenyewe ndiyo huwa wananishobokea kutokana na uigizaji wangu,” amesema Mzee Majuto.
Hivi karibuni, Mzee Majuto alidaiwa kuoa binti mdogo ambaye ni sawa
na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18 akidai kuwa sheria ya dini
inamruhusu kufunga ndoa na wake wanne.
Nkupamah blog



0 comments :
Post a Comment