Msumbiji Yahalalisha Mapenzi Ya Jinsia Moja

Thursday, July 2, 2015

Nkupamah blog

Nchi ya Msumbiji imepitisha sheria inayohalalisha mapenzi ya jinsia moja, na kuwa miongoni mwa nchi chache Barani Afrika zinazoruhusu mapenzi ya jinsia moja.
 
Sheria hiyo iliyowekwa na wakoloni wa nchi hiyo, Ureno awali ilifutwa na Bunge la nchi. Watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja, wametaja hatua hiyo kama ushindi mkubwa.
 
Hata hivyo nchi nyingi za Afrika zimeweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja. Nigeria ilipiga marufuku na kuweka adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakati huo Uganda nayo imeapa kurejesha sheria kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja. Sheria ya awali ilitupiliwa nje na mahakama ya kikatiba.
 
Msumbiji sasa anajiunga na mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na Afrika Kusini ambapo siyo hatia kuwa mpenzi wa jinsia moja.
 Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment