Katibu
wa itikadi na uenezi Nape Nnauye amesema vikao hivyo vilianza leo kwa
sekretalieti kukutana na kujadili maandalizi ya kamati kuu (CC),
Halmashauri Kuu (NEC) na mkutano mkuu huku kesho julai 8 inakutana
kamati ya Usalama na maadili ndani ya Chama ambacho kitakuwa chini ya
Mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania
Jakaya Kikwete.

Nape
amesema keshokutwa Julai 9 kutakuwa na uzinduzi wa Ukumbi mpya ambako
kutafanyikia Mkutano mkuu wa mwaka huu utakaofanywa na mwekiti wa CCM
Jakaya Kikwete na mchana kutakuwa na kikao cha kamati kuu ya halmashauri
ya taifa ya chama hicho ambacho ni moja ya vikao kuelekea mkutano mkuu.
Julai
10, kutakuwa na kikao cha NEC kitakateua jina la mgombea urais wa
Zanzibar , kazi ya pili itapia irani ya taifa ya CCM itakayotumika
kuombea kura na kutumiwa kwa mwaka 2015/20 na kazi ya tatu kamati hiyo
itapokea majina matano yatakayokuwa yameteuliwa na NEC na kisha
kuyapigia kura ili kupata majina matatu ambayo yatapigiwa kura kwenye
mkutano mkuu ili kupata jina moja litakalogombea nafasi ya urais mwaka
huu.
Alisema
Julai 11 itakuwa siku ya mkutano mkuu ambao unatarajiwa kuonyeshwa moja
kwa moja na vyomba mbalimbali vya habari zikiwemo Television na Radio
0 comments :
Post a Comment