Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku
mbili zijazo.
Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.
Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza
hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata
rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje
rufaa,” alisema Nape.
Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka
kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama
hicho.
Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.
Kwa mujibu wa ratiba ya
kikao,Kamati Kuu itakutana tarehe tisa na kutoa wagombea watano kabla
ya Halmashauri Kuu kukutana tarehe 10mwezi huu, ambapo majina matatu ya
wagombea yatateuliwa kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu
tarehe 11 ili kumpata mgombea mmoja atakaepeperusha bendera ya chama
hicho.
MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment