Katika kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzielekeza Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya maendeleo kuona hali halisi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini mafanikio na changamoto na hatimaye kutoa ushauri katika ngazi husika kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Moja ya Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Miradi imeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na ile ya Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika mfumo wa kimaabara.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (wa nne kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na
Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa
kwanza kushoto) na maafisa kutoka kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
pamoja na wataalam wa Mradi wa Kituo cha Kuzalisha Samaki kilichopo
Kingolwira Mkoani Morogoro wakiangalia sehemu maalum ya kukuzia
vifaranga vya samaki baada ya kutotoleshwa.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence
Mwanri (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na
Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa
kwanza kulia) pamoja na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Dodoma,
hatua ulipofikia na changamoto zilizopo kutoka kwa Mtaalamu Elekezi wa
mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia).
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi. Florence
Mwanri (wa tatu kulia) akiangalia kazi ya ujenzi wa barabara ya Iringa –
Dodoma inavyoendelea wakati alipotembelea mradi huo pamoja na maafisa
kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Pamoja nao ni Mtaalamu Elekezi wa
mradi Bw.Robin de Kock (mwenye kofia katikati).
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa pili kushoto)
pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipewa maelezo
kuhusu bwawa la kuzalisha umeme la Mtera kutoka kwa Meneja wa Kituo Bw.
Abdallah Ikwasa (wa nne kushoto). Hii ni sehemu ambapo uzalishaji wa
umeme unafanyika. Bwawa la Mtera linapatikana katika mikoa ya Iringa na
Dodoma. Lina uwezo wa kuzalisha MW 80 ambao unaoingizwa katika Gridi ya
Taifa.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (wa kwanza kushoto) na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakipata maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa reli kutoka Kitaraka
hadi Malongwe mkoani Tabora kutoka kwa Bw. Raphael Mwandumbya (mwenye
kofia) ambaye ni Mkaguzi wa ujenzi wa reli hiyo. Mradi huu ni sehemu ya
ujenzi na ukarabati unaoendelea katika Reli ya kati ambao una urefu wa
kilometa 89.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (wa pili kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na
Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omari Abdallah (wa
kwanza kushoto) na maafisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakiangalia uharibifu wa barabara ambao unafanywa na wananchi wasio
waaminifu kwa kuchota kokoto pembezoni mwa barabara hiyo ambayo bado
inaendelea kujengwa. Barabara hii inajengwa na Nicholas O’Dwyer &
company Ltd Consulting Engineers ambapo kipande cha Manyoni hadi Itigi
kipo katika hatua za mwisho kukamilika. Lengo la mradi ni kuendelea
kujenga barabara ya Manyoni – Itigi kwa kiwango cha lami katika sehemu
tatu za utekelezaji ambazo ni: Manyoni – Itigi – Chaya (KM 89.35), Chaya
- Nyahua (KM 90), na Nyahua – Tabora (KM 85).
Jengo kwa ajili ya kutolea huduma za mpakani (One Stop Border Post)
Mtukula, mradi ambao unahusisha ujenzi wa miundombinu inayosaidia
utolewaji wa huduma bora na za kisasa mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Lengo la mradi wa One Stop Border Post ni kukamisha vituo vya utoaji
huduma za pamoja mipakani kati ya Tanzania na nchi za jirani.
Timu ya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiongozwa na
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (wa tatu kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa wataalam
wanaohusika na Mkongo wa Taifa. Lengo la mradi kwa mwaka 2014/2015 ni
mapitio ya miundombinu ya Mkongo na mifumo kwa ajili ya maboresho,
ujenzi Awamu ya III sehemu ya kwanza ya upanuzi wa mkongo kwa maeneo
yaliyobaki katika awamu I na II na uhakiki wa ubora wa Mkongo.
Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence
Mwanri (wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara Mipango na
Ufuatiliaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bw. Omary Abdallah (wa
kwanza kulia) na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakipata
maelezo kuhusu mafanikio na changamoto za Mradi wa Ranchi ya Taifa
Misenyi kutoka kwa Meneja wa Mradi Bw. Martin Ladislaus (katikati).
Shamba hili la mifugo lipo Karagwe, mkoa wa Kagera. Ni moja kati ya
mashamba makubwa 9 nchini ya uwekezaji, limepimwa na kupata hati miliki.
Ujumbe kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ukiongozwa na Naibu
Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bibi. Florence Mwanri
(mwenye t’shirt nyeusi) wakiangalia sehemu ya kuogeshea ng’ombe.
Wengine ni Meneja wa Mradi Ranchi ya Taifa Misenyi, Kagera Bw. Martin
Ladislaus (wa tatu kulia) na Meneja wa Mradi Ranchi ya Kitengule, Kagera
Bw. Hemedi M. Seif (wa pili kulia).



0 comments :
Post a Comment