Dhima
yetu ya kuendeleza mabadiliko ndani ya Simba bado inaendelea kushika
kasi, Katika kipindi cha miezi mitatu sasa, mmekuwa mashuhuda wa Simba
inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika jinsi mpira unavyoendeshwa,
kujali wanachama, wapenzi wake na kukuza vyanzo vya mapato.
Akizungumza
na waandishi wa habari Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Katika
kukuza wigo wake wa kuwashirikisha wapenzi wake katika kuleta maendeleo
ya klabu Simba Sports Club inazindua makakati wa kuwashirikisha wapenzi
wenye nia ya kuwa chachu ya maendeleo kwenye klabu yao. Simba ni klabu
ya wanachama na wapenzi wa Simba, hili ndilo jambo la msingina kujivunia zaidi.
Kwa msingi huu wigo wetu wa wapenzi nimtaji muhimu katika kuetekeleza malengo mbalimbali ya klabu ya Simba. Hivyo basi leo hii klabu ya Simba inazindua rasmi Mabalozi wa Simba, hawa ni wapenzi wa Simba ambao wako tayari kushirikiana na klabu katika kuleta maendeleo ya klabu yetu’’.
Aveva
aliendelea kusema ‘’ Katika ahadi zetu wakati wa uchaguzi tuliahidi kuwa
tumenuia kwa dhati kuleta mapinduzi ya kimaendeleo ndani ya Simba.
Napenda kusema safari yakuendelea kuifanya Simba kuwa klabu bora ndani
na nje ya uwanja imepamba moto. Kwa uhakika malengo mengii kiwemo la
kujenga uwanja na kambi ya mazoezi ya Simba sio ndoto. Kupitia mabalozi
wa Simba na mikakati yetu mingine ya utunishaji wa mapato tunaamini
kwa dhati malengo yetu tutayafikia.
Kihistoria
Simba imekua ni timu yenye kutendana kufikiriki maendeleo na kutumia
nguvu za wapenzi na wanachama, tulianza kwa kuwawa kwanza kujenga jengo
la klabu, Mzee Dalali aliona mbali na kununua uwanja Bunju, nasisi
tutaanza ujenzi, hii ndio dhima ya uongozi ndani ya Simba kupokezana
vijiti vya maendeleo’’.
Kwa
upande wake MkurugenziMtendajiwa EAG Group LTD ambao ni washauri
watekelezaji wa mikakati ya biashara na masoko wa Simba ImaniKajula
alisema ‘’Zoezi la kuteua mabalozi wa Simba ni endelevu na litafika
kila kona ya Tanzania. Hawa ni mashabiki ambao mawazo, michango yao ya
hali na mali, kutumia ushawishi wao kutaleta maendeleo kwenye klabu
yetu. Hawa watakuwa mstari wa mbele kwenye Simba Week kuhamasisha
ufanyaji kazi za jamii na kushiriki kwa wapenzi na wapenda maendeleo
katika kusukuma maendeleo ya Simba.
Napenda
kuwashukuru sana Mabalozi hawa kwa kutenga muda na kuwa tayari kusaidia
juhudi za kuiletea Simba maendeleo. Uongozi wangu utakuwa bega kwa bega
nanyi katika kazi hii adhimu.


0 comments :
Post a Comment