.Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta
akikabidhiwa msaada wa madawati 100 na Meneja Biashara wa Benki ya KCB
Tanzania, Tawi la Mlimani City, Benjamin Mgonja(kushoto) wakati wa hafla
fupi iliyofanyika shuleni hapo.Benki hiyo imetoa msaada wa matawati
1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja
na walimu wa shule ya msingi Tabata.Wakati wa hafla ya kukabidhiwa
msaada wa madawati 100 na Benki hiyo jana.
Baadhi
ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Tabata wakibeba
madawati kuyapeleka madarasani baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati
100 na benki ya KCB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mradi wa madawati 1000
kwa shule za msingi 10 za msingi jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta(kushoto)akiteta jambo na Meneja
Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City Jijini Dar es
Salaam, Benjamin Mgonja wakati wa hafla fupi ya makabidhino
ya msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na
kampeni yake ya kutoa msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini
Dar es Salaam.
.Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Msingi Tabata jijini Dar es Salaam,
wakionyesha mshikamano na furaha baada ya kupokea msaada wa madawati 100
kutoka Benki ya KCB Tanzania wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni
hapo jana.
0 comments :
Post a Comment