…………………………………
MKURUGENZI wa Msama Promotions,
Alex Msama amewaita Maaskofu na viongozi wengine wa dini katika
uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji nguli Bonny Mwaitege zinazotarajia
kuzinduliwa Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa Msama ambaye ni
mdhamini wa uzinduzi huo, Maaskofu watafikisha ujumbe wa neno la
Mungu kwa karibu zaidi baada ya waimbaji kumaliza kazi yao jukwaani.
Msama alisema uzinduzi huo
unatarajia kusindikizwa na waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje lengo
likiwa ni kufanikisha uzinduzi mahiri wa albamu hizo.
Msama alisema pamoja na uzinduzi
huo kusindikizwa na waimbaji mahiri pia, waimbaji chipukizi
watamsindikiza Mwaitege ambaye hivi sasa anaendelea na mazoezi kuelekea
uzinduzi huo.
Aidha Msama alisema hivi sasa
muimbaji huyo pia anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye
albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Nairobi.
Msama alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa injili kujiandaa na uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake.
“Maandalizi makubwa kuelekea
uzinduzi wa Mwaitege yameshafanyika, kilicho mbele ni uzinduzi wa hali
ya juu, mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema Msama na kuongeza.
“Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni
wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa sababu yamefanywa kwa ustadi
mkubwa, mashabiki watarajie kazi bora zaidi kutoka kwa muimbaji huyo,”
alisema.
Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo
mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, Fungua Moyo wako,
Njoo uombewe na Yesu yupo.
0 comments :
Post a Comment