Waziri
wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdala Kigoda akizungumza katika uzinduzi
wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua
Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la
Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya
nchini Cuba.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza
Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki
kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na
Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda
hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano
na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Baadhi ya wageni mbalimbali waalikwa walioshiriki katika hafla ya
uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa
Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Waziri Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm akizungumza katika uzinduzi
wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Waziri Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm (wa nne kushoto) pamoja na
Rais Jakaya Kikwete (wa tano kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
HOTUBA
YA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA WAKATI WA UFUNGUZI WA KIWANDA CHA KUZALISHA VIUADUDU VYA
KUULIA VILUWILUWI VYA MBU WANAOENEZA MALARIA KILICHOPO KATIKA ENEO LA
VIWANDA LA TAMCOKIBAHA, PWANI
TAREHE 2 JULAI, 2015
Mheshimiwa Hailemariam Desalegm, Waziri Mkuu wa Ethiopia;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Mheshimiwa Dkt. Abdala Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara;
Mheshimiwa Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii;
Ndugu Lobani Gutieres Ravelo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya LABIOFAM, Cuba;
Ndugu Joyce Phumaphi, Katibu Mtendaji wa ALMA;
Mheshimiwa Lorge Luis Lopez Tarmo, Balozi wa Cuba nchini Tanzania;
Mheshimiwa Evarist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani;
Waheshimiwa
Mabalozi wa Nchi za Nje na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa;
Wageni Waalikwa;
Wanahabari;
Mabibi na Mabwana;
Ni furaha iliyoje kwangu kuwepo hapa leo, kushuhudia uzinduzi wa Kiwanda
cha Kutengeneza Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu. Furaha yangu
inaongezeka zaidi kwa kuwepo ugeni mkubwa wa Waziri Mkuu wa Ethiopia,
Mheshimiwa Hailemariam Desalegn. Yeye ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa
Viongozi wa Afrika walio mstari wa mbele katika Mapambano Dhidi ya
Malaria katika Bara la Afrika (ALMA).
Kwa
niaba ya Watanzania wenzangu wote namshukuru sana mgeni wetu kwa
kutenga muda wake na kusafiri kutoka Ethiopia kuungana nasi siku ya leo.
Ujio wako unaweka uzito mkubwa kwenye azma yetu hii ya kutokomeza
Malaria katika Bara letu.
Pamoja nasi, napenda pia kuwakaribisha watu wafuatao; kwanza, Ndugu
Alfred Romberto Corta, Rais wa Kampuni ya LABIOFAM ya Cuba waliotuuzia
teknolojia ya kutengeneza dawa hizo. Wa pili, ni Bibi Joy Pumaphi,
Katibu Mtendaji wa ALMA. Mwisho, ingawaje siyo mwisho kwa umuhimu wageni
wote wengine waliopo hapa leo.
Chimbuko la Kiwanda
Wageni waalikwa;
Chimbuko la ujenzi wa kiwanda hiki ni ziara yangu niliyoifanya nchini
Cuba mwezi Desemba, 2009.
Katika
ziara ile, mwenyeji wangu Rais Raul Castro alinipangia ratiba ya
kutembelea Kiwanda cha LABIOFAM kinachomilikiwa na Serikali ya Cuba na
kinachozalisha dawa za viluwiluwi vya mbu wanaosababisha malaria. Baada
ya kuvutiwa na maelezo na teknolojia ile na kuhakikishiwa kuwa haina
athari kwa mazingira na afya ya binadamu niliagiza mambo mawili
yafanyike. Kwanza, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iagize dawa hizo
kutoka Cuba zitumike nchini; na Pili, Shirika la Taifa la Maendeleo
(NDC) lianzishe ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM kwa lengo la kujenga
kiwanda cha aina hiyo hapa nchini.
Shukurani kwa Serikali ya Cuba.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda cha
Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda
hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano
na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.[/caption]
Mabibi na Mabwana;
Shukrani zangu za pekee zimuendee Mheshimiwa Raul Castro, Rais wa
Jamhuri ya Kisoshalist ya Cuba, na rafiki mkubwa wa Tanzania, kwa
kukubali kutuuzia teknolojia hii. Wenzetu wa Cuba wametufaa sana kwani
“hawajatupa tu samaki, bali wametupa ndoano ya kuvua samaki”.
Wangeliweza kabisa kwa tamaa kukataa kutuuzia teknolojia na ujuzi wao na
kutaka kutuuzia dawa. Pamoja na kuwa wao si nchi tajiri hawakufanya
hivyo.
Wameshirikiana
nasi katika ujenzi na kukubali kutupa wataaalam ambao watabakia nchini
kwa miaka mitano kufundisha watu wetu na kutusaidia kwa masuala ya
kiufundi na kitaalam. Tunaye pamoja nasi kiongozi na Mhandisi Mkuu
aliyesimamia ujenzi huu Ndugu Alfredo R. Drespo Dorta ambaye amesafiri
toka Cuba kuja kushuhudia ufunguzi wa kiwanda hiki. Huu ndio urafiki wa
kweli na udugu. Nakuomba Mheshimiwa Balozi wa Cuba unifikishie shukrani
zangu za dhati na za Watanzania wenzangu kwa Rais Raul Castro na kwa
ndugu zetu wananchi wa Cuba.
Vita
Dhidi ya Malaria
Mabibi na Mabwana;
Leo tunapiga hatua kubwa na ya aina yake katika vita yetu dhidi ya
malaria hapa nchini na katika Bara la Afrika hasa nchi zilizo Kusini mwa
Jangwa la Sahara. Katika Ripoti ya Malaria Duniani ya mwaka 2014
iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa, mwaka
2013, malaria ilisababisha vifo vya watu 584,000. Kati ya vifo hivyo
asilimia 90 vilitokea barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Bahati
mbaya sana waathirika wakubwa walikuwa ni wanawake na watoto chini ya
umri wa miaka 5.
Inakadiriwa
pia kwamba malaria inazigharimu nchi wastani wa asilimia 40 ya fedha
zao za bajeti ya afya na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi wa baadhi ya
nchi za Afrika kwa asilimia 1.3.
Waziri Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm (kushoto) pamoja na Rais
Jakaya Kikwete (kulia) wakizinduwa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu
vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya
LABIOFAM ya nchini Cuba.[/caption]
Kinachosikitisha zaidi ni ule ukweli kwamba, upo uhusiano mkubwa kati ya
malaria na umasikini. Bahati nzuri ugonjwa huu unazuilika na kutibika
maana uliwahi kuwa tishio kubwa duniani lakini leo ni tishio zaidi
Afrika. uzoefu wa nchi nyingine duniani waliofanikiwa kuzuia na
kutokomeza. Unatupa matumaini kuwa na sisi tukiiga mifano yao tunaweza
kuwa kama wao. Kuwekeza katika kiwanda cha aina hii kutatuwezesha
kutokomeza malaria.
Hali ya Malaria Nchini
Mabibi na Mabwana;
Baadhi ya viongozi na wageni waalikwa wakiwasili katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho.
Tangu
mwanzoni mwa uongozi wangu kupambana na malaria tuliupa kipaumbele cha
juu. Ndicho chanzo cha wagonjwa wengi na vifo vingi nchini. Tumekuwa
tunafanya mambo makuu matatu katika kupambana na malaria; kwanza,
kutumia dawa mseto kutibu wagonjwa wa malaria. Pili, kuhamasisha
matumizi ya vyandarua vilivyopuliziwa dawa na tatu, kupulizia dawa
inayoua mbu ndani ya nyumba. Kwa kufanya hivyo tumefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kupunguza wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria. Kiwango cha
maambukizi nacho kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi asilimia
10 mwaka 2012. Vifo vitokanavyo na malaria kwa uzazi vimekupungua kutoka
41 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2004 hadi 12 kwa vizazi hai 100,000
mwaka 2014. Idadi ya wagonjwa chini ya miaka 5 imepungua kutoka wagonjwa
milioni 5,372,569 mwaka 2004 hadi wagonjwa milioni 3,486,326 mwaka 2014
na vifo vya watoto wa miaka 5 kwenda chini vimepungua kutoka 7,907
mwaka 2004 hadi 4,008 mwaka 2014. Kwa ujumla idadi ya wagonjwa wote
imepungua kwa asilimia 51 na vifo kwa asilimia 71 kati ya 2004 na 2014.
Kwa upande wa matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa, Serikali
imesambaza vyandarua 26,371,329 nchi nzima, yaani vyandarua viwili kwa
kaya, kwa watoto wa umri wa chini ya miaka 5 na kina mama wajawazito.
Matokeo yake, idadi ya matumizi ya vyandarua vilivyotiwa dawa
imeongezeka kutoka asilimia 23 mwaka 2004 hadi asilimia 92 mwaka 2012.
Kwa upande wa wajawazito kutoka asilimia 27 mwaka 2004 hadi asilimia 75.
mwaka 2014. Kwa upande wa watoto wa miaka 5, idadi imeongezeka kutoka
asilimia 26 mwaka 2004 hadi asilimia 72 mwaka 2014.
Mafanikio zaidi makubwa na ya kujivunia yamepatikana Zanzibar. Kiwango
cha maambukizi ya malaria kimeshuka na kufikia asilimia 0.2 hivi sasa.
Pamoja na kufanya yale mambo matatu ndugu zetu wa Zanzibar walipulizia
na kuua viluwiluwi vya mbu waenezao malaria. Kama imewezekana Zanzibar
inatufanya tuamini kuwa itawezekana na huku Bara pamoja na ukubwa wa
eneo na wingi wa watu. Ni kwa sababu hiyo, tulichukulia uwekezaji huu wa
kiwanda cha kuzalisha viuatilifu kuwa uwekezaji wa kimkakati katika
vita dhidi ya malaria. Kwa kuwa sasa dawa hizi zitakuwa zikizalishwa
nchini kwa wingi na gharama nafuu, jukumu letu sasa ni kuanzisha kampeni
nchi nzima ya kupulizia maeneo yote ili kuua viluwiluwi vya mbu pale
wanapozaliwa. Sasa tunatangaza vita si tu na mbu bali na viluwiluwi
vyake.
[caption id="attachment_59103" align="aligncenter" width="759"]
Rais Jakaya Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Desalegm wakiwa wamesimama kuimba nyimbo za taifa la Tanzania na
Ethiopia katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu
vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya
LABIOFAM ya nchini Cuba.
Maelekezo Mahsusi
Waziri
Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm akizungumza katika uzinduzi wa
Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini
Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)
kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.
Mabibi
na Mabwana;
Natoa pongezi kwa Bodi ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa
kusimamia vizuri ujenzi wa kiwanda hiki. Jukumu kubwa na lililo mbele
yenu sasa ni kuhakikisha kiwanda hiki kinazalisha na kujiendesha
kibiashara. Hatutarajii kiwanda hiki kiijiendeshe kwa hasara maana
biashara yenyewe ni ya uhakika ndani na nje ya nchi yetu. Kama
nilivyokwishasema hapo awali, Tanzania ni mwanachama, tena mwanachama
mwanzilishi wa Umoja wa Marais wa Afrika walio katika Mapambano Dhidi ya
Malaria (ALMA).
Umoja
huu una nchi 49 Sote kwa pamoja, tunayo dhamira ya kuondokana na
malaria katika nchi zetu na tumejiwekea malengo. Uwepo hapa wa
Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia ni ushahidi huo.
Shirikianeni na Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutangaza
bidhaa za kiwanda hiki. Tafuteni masoko barani Afrika, maana,
kutokomeza malaria hakutegemei mafanikio katika nchi yetu tu, bali pia
na kwa nchi nyingine katika Bara letu.
Naelekeza
pia ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kukitumia kiwanda hiki katika mipango yake ya kutokomeza malaria katika
Halmashauri zetu. Halmashauri zihamasishe watu wetu na kaya zilizo
kwenye maneo yao ya utawala kutumia dawa zinazozalishwa na kiwanda hiki.
Angalieni namna bora ya kuwezesha hilo kufanyika.
Kwa
kupulizia dawa hizi na kutokomeza viluwiluwi wa mbu kutang’oa mzizi wa
fitina unaosababisha maambukizi na vifo vya malaria.
Hitimisho
Mabibi na Mabwana;
Kama nilivyosema awali, leo ni siku ya furaha sana kwangu kwa kukamilika
kiwanda hiki na kupata fursa ya kushuhudia ufunguzi wake. Mafanikio
tuliyoyapata katika kutibu malaria ni makubwa na ya kutia moyo. Hata
hivyo, mafanikio hayo yasingekuwa endelelevu iwapo tusingeongeza nguvu
na mkazo katika kukinga na kuzuia maambukizi.
Kiwanda
hiki tunachokifungua leo kitaimarisha uwezo wetu wa kukinga na kuzuia
maambukizi ya malaria. Wahenga wamesema daima “kinga ni bora kuliko
tiba”. Sasa tuna uhakika kuwa mapambano yetu dhidi ya malaria
tumeyafikisha mahali pazuri. Nafurahi kuona leo tunatamka kwa vitendo
kuwa “Malaria Haikubaliki”. Sasa natangaza kuwa kiwanda cha Kuzalisha
Viuadudu vya Viluwiluwi vya Mbu kijulikanacho kama Tanzania Biotech
Products Limited kimefunguliwa rasmi.
Asanteni kwa kunisikiliza!


0 comments :
Post a Comment