2015 tumeshuhudia mastaa mbalimbali wa kike na wa kiume Tanzania
wakitangaza nia ya kuingia bungeni akiwemo mwimbaji wa Taarab Mzee
Yusuf, Profesa Jay, Steve Nyerere na kwa Wanawake waliojitokeza
kuziwania nafasi za Ubunge wa viti maalum ni pamoja na waigizaji Wema
Sepetu na Wastara, na msanii wa bongofleva Ksher.
Wema Sepetu na Wastara hawakupita kutokana na kukosa kura za kutosha
lakini Khadija Shaaban (Ksher) amepita tena ambapo alithibitisha hayo na
wakati mwingi kwenye maneno yake ya kujinadi ni ‘mara nyingi watu
wanakosa uthubutu kutokana na kutojiamini kuwa vile walivyo wanaweza
kufanya mambo makubwa ya ajabu bila kujali kiwango cha elimu, pesa au
mtandao alionao’
Kwa upande wa Wastara, kwenye kura za maoni zilizopigwa akiwania Ubunge
wa viti maalum kupitia Walemavu, zilipigwa kura 759, zikaharibika 40
huku Magreth Mkanga akipata kura 424, Wastara akishika nafasi ya pili
kwa kuchukua kura 254 na Chausiku Lukinga 43.
Source:Millard ayo.com


0 comments :
Post a Comment