Mbunge Ataka Wanaokamatwa Na Na Madini ya Tanzanite Wauawe

Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma (CUF), ameitaka serikali kuwaua watu watakaokamatwa na madini ya Tanzanite.

Amesema pamoja na serikali kuzungushia ukuta machimbo ya madini hayo Mirerani, mkoani Arusha njia pekee ya kukabiliana na watoroshaji hao ni kuyaweka katika orodha ya nyara za serikali ili watakaokamatwa nao wauawe.

Nachuma ameyasema hayo jana Mei 31, bungeni jijini Dodoma, alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/19.

“Lakini pia serikali inunue mashine za kuchakata madini ya Tanzanite nchini badala ya uchakataji huo kufanyika nje ya nchi ikiwamo India ambako madini hayo yamesababisha ajira laki sita,” alisema.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Viti Maalumu Catherine Magige aliitaka serikali ifanye kila linalowezekana katika kudhibiti utoroshwaji wa madini ya Tanzanite kwa kuwa bado yanatoroshwa nchini ijapokuwa kuna ukuta umejengwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment