Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati
na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe akisaini kitabu cha wageni
mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi – Kilimanjaro
kabla ya kuanza kwa uendeshaji wa mafunzo ya huduma za leseni kwa
njia ya mtandao. Mafunzo hayo yanahusisha wachimbaji wa madini lengo
likiwa ni kuwapa uelewa wa matumizi ya huduma za leseni kwa njia ya
mtandao
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati
na Madini, Kitengo cha Leseni Charles Gombe akielezea mikakati ya
Wizara katika uboreshaji wa huduma za leseni kwa wachimbaji wa madini
(hawapo pichani) katika mafunzo yaliyofanyika wilayani Same mkoani
Kilimanjaro
Baadhi ya wachimbaji wa madini
kutoka wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wakifuatilia kwa makini mada
zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini
(hawapo pichani)
Mmoja wa wachimbaji wa madini kutoka wilayani Same, mkoani Kilimanjaro Richard Mbwambo akiuliza swali katika mafunzo hayo
Afisa Madini Mkazi, Mkoa wa
Kilimanjaro, Fatuma Kyando akielezea sheria na kanuni za uchimbaji wa
madini nchini katika mafunzo hayo
Mmoja wa wachimbaji wadogo, Naamin Samuel kutoka kampuni ya Kivoroi na Ndarauoi akiuliza swali katika mafunzo hayo
Wataalam kutoka Wizara ya
Nishati na Madini ( waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na
washiriki wa mafunzo hayo waliosimama nyuma.
Baadhi ya watoto kutoka
wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakipozi katika picha ya pamoja mbele
ya gari la matangazo la Wizara ya Nishati na Madini lililokuwa
linatumika wakati wa zoezi la uhamasishaji wa matumizi ya huduma za
leseni za madini kwa njia ya mtandao.
0 comments :
Post a Comment