Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha Aachiwa Kwa Dhamana

Wednesday, August 26, 2015

@nkupamah blog

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Masha alifikishwa mahakamani hapo jana nyakati za saa 6:49 mchana na kuhifadhiwa mahabusu na ilipofika saa 9:31 alasiri alipelekwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Waliarwande Lema kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana.

Masha aliachiwa huru baada ya nyaraka za wadhamini wake wawili wanaoaminika ambao kila mmoja alisaini bondi ya Sh 1milioni kuhakikiwa na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kuithibitishia mahakama kuwa nyaraka hizo ni halali.

Kufanyika kwa uthibitisho huo wa nyaraka za wadhamini ndio uliopelekea jana Masha kupelekwa mahabusu katika gereza la Segerea.

Baada ya kumaliza kukamilisha taratibu hizo za dhamana ilipofika saa 9:46 alasiri Masha, mkewe, mawakili wanaomtetea katika kesi hiyo, Peter kibatala na Albart Msando pamoja na ndugu zao wengine waliondoka mahakamani hapo kwenda nyumbani.

Awali Agosti 25, 2015 Masha alipandishwa kizimbani akikabiliwa na shtaka la kutumia lugha ya matusi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi.

Masha aliyekuwa amevaa tisheti jeusi, suruali ya jinsi ya rangi ya Bluu na viatu aina ya Sendo anadaiwa kuwa Agosti 24,2015 katika kituo cha polisi cha Osterbay alitoa lugha ya matusi kwa maofisa wa jeshi la polisi.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment