DART yakanusha taarifa potofu kuhusu mabasi yaendayo haraka Dar


Kuna upotoshaji wa makusudi uliozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mabasi yaliyozinduliwa tarehe 17/08/2015 kuwa.
1. Ati ni ya Kichina


2. Milango ya kushukia na kupandia abiria iko kushoto hivyo hayaendani na miundombinu iliyojengwa.

HUO NI UZUSHI WENYE LENGO LA KUWAPOTOSHA WATANZANI WALIOCHOSHWA NA MSONGAMANO UNAOONGEZEKA SIKU HADI SIKU
TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA HII HAPA:
1. Kiwanda kilicho assemble (Kuunganisha) mabasi haya kinaitwa Golden Dragon cha China.(P.T)
2. Aina ya injini ni CUMMINS ya Marekani (USA)

3. Aina ya giaboksi ni VOITH ya Ujerumani.

4. Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani.

5. Mgumo wa difu ni kutoka Marekani (USA).

6. Aina ya suspension (za upepo) Air Suspension kutoka Marekani (USA).

7. Mfumo wa breki ni WABCO

8. Aina za mabasi ziko mbili. Articulated mita kumi na nane almaarufu (Ikarusi) kutoka Hungary zitakazopita kwenye barabara Maalumu za zege zilizojengwa na Mabaai ya mita kumi na mbili yanayoitwa (Feeder) Mabasi Mlisho yatakayotumia vituo vilivyoko nje ya mfumo mfano kituo cha Shekilango, Morocco Hotel, Mwanamboka na Magomeni Mapipa kuwapeleka na kuwaleta kwenye mfumo.

9. Milango ya kupanda na kushukia abiria ipo kulia na kushoto ili kukidhi mahitaji ndani na nje ya mfumo ambayo idadi yake ni minne kila upande ila itatumika mitatu na mmoja niwa dharula kila upande.

10. Urefu kutoka ardhini kwa milango ya kushoto ya basi ni sentimita thelathini (30) ambayo hata mtoto anaweza kushuka bila msaada wa mtu mzima.

11. Urefu wa milango ya kulia ni sentimita tisini (90) sawa na urefu wa platform za kila kituo cha DART unaomuwezesha hata mtu mwenye mahitaji maalum Kuingia na kutoka ndani ya basi bila msaada wa mtu.

12. Ndani ya basi kuna eneo la kukaa watu wenye mahitaji maalum - walemavu, wazee na mama wajawazito.

13. Mfumo wa ulipaji nauli unafanyika vituoni kama ilivyo kwenye kivuko pale Kivukoni hivyo basi hili halina Kondokta. Makondakta wapo vituoni.

14. Muda wa safari kutoka Kivukoni hadi Kimara ni wastani wa dakika thelathini (30) ikihusisha muda wa kushusha na kupakia kwenye vituo vya DART.

15. Ni marufuku kwa chombo ama mwananchi kutumia barabara maalum za mabasi. Wananchi watumie maeneo yaliyotengwa maalum kulingana na mahitaji. Watumiaji wa bodaboda wanatakiwa kupita kwenye barabara zinazotumiwa na magari ya kawaida na siyo eneo lililotengwa kwa ajili ya watembea kwa miguu.
HIZI NDIZO TAARIFA MUBIMU NA RASMI KWA WATANZANIA
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment