Mji wa Tanga ni Mji Mkuu wa Mkoa wa Tanga uliopo ufukweni mwa Bahari ya
Hindi. Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehemu ya kaskazini mwa
Tanzania. Njia ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.
Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka;
Bonde lenye rutuba;
Barabara upande wa mto na
Shamba juu ya mlima.
Neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni wenyeji wa mkoa huo lina maana ya shamba, wao hulitamka N'tanga.
Tanga insaemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya
14 KK. Mji wa Tanga haukupata umuhimu kama mji wa jirani ya Mombasa.
Tarihi ya Pate inasema ya kwamba kabla ya kuja kwa Wareno., Pia Pate
iliwahi kutawala Lindi kwa muda fulani.
Katika karne ya 19 KK, Tanga ilikuwa chini ya utawala wa Omani na
Zanzibar. Misafara ya biashara imeanzishwa hapa kwenda bara. Kutokana na
bandari yake nzuri ya kiasili Tanga ilikua sana wakati wa ukoloni wa
Wajerumani waliojenga bandari ya kisasa pamoja na reli kwenda Moshi.
Reli iliwezesha kilimo kwa ajili ya soko la dunia na Tanga ikawa bandari
kuu kwa ajili ya katani na kahawa. Baada ya Uingereza kuchukua utawala
wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa
na ile ya kati hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia.
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Tanga iliona mapigano makali tar. 3
- 5 Novemba 1914. Jaribio la Uingereza kuvamia Tanga kwa kikosi cha
maaskari 8000 Waingereza na Wahindi kutoka meli kwenye Bahari Hindi
Lilishindwa vibaya na Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa
Paul von Lettow-Vorbeck.
Mwaka 1922 "Tanganyika Territory African Civil Services Association"
(TAA) iliundwa Tanga ambayo ilikuwa shirika ya kwanza ya Kiafrika yenye
shabaha za kisiasa.
Kutokana na kupanuka kwa bandari ya Dar-es-salaam, umuhimu wa bandari ya Tanga umerudi nyuma.
0 comments :
Post a Comment