Bomoa bomoa Ingine Yaja Dar

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi  amewataka wananchi waliojenga nyumba pembezoni mwa barabara ya Afrikana- Salasala Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, kubomoa  nyumba zao kupisha ujenzi wa mitaro.
Akizungumza leo Alhamisi Januari 11, katika ziara ya kukagua barabara za Wilaya ya Kinondoni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, Hapi amesema barabara hiyo imeharibika kutokana na kutokuwa na mitaro hiyo ya kupitisha maji.
Amesema uchimbaji wa mitaro hiyo umekuwa mgumu kwa kuwa nyumba hizo zimejengwa karibu na barabara, huku akiahidi  kuanza ujenzi baada ya wiki tatu kuanzia leo.
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini kuwa wamiliki wa nyumba hizo watalazimika watabomoa sehemu ya nyumba zao kutokana na nyingi kuingia katika eneo la barabara kwa kiasi kidogo.
“Mvua ikinyesha maji yanapita katikati ya barabara na kuifanya iharibike mara kwa mara. Hii inatokana na kukosekana kwa mitaro. Niwaombe muwe wavumilivu ili kuondokana na kero,” amesema na kuongeza,
“Namuagiza  meneja wa Tarura (Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini) kuanza ujenzi wa kilomita moja kati ya 3 ili kuondokana na kero hii lakini kwa wakazi waliovamia barabara waondoke wenyewe" amesema Hapi.
Amesema Serikali haina pesa ya kuwalipa waliojenga kando ya barabara hiyo pindi watakapobomoa nyumba zao.
“Tunawaomba wabomoe wenyewe la sivyo watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kulipa gharama zote za ubomoaji,” amesema.
Meneja wa Tarura Manispaa ya Kinondoni, mhandisi Leopold Runji amesema  maelekezo aliyoyatoa Hapi yatatekelezeka, kuwataka  wakazi hao waliovamia barabara kuondoka.
Mbali na barabara hiyo,  pia ametembelea barabara ya Ardhi-Makongo hadi Goba yenye urefu wa kimomita 4 inayojengwa na Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Dar es Salaam itakayogarimu Sh9.1bilioni.
Meneja waTanroads mkoani Dar es Salaam, mhandisi Saimon Mgani amesema changamoto wanazokutana nazo katika mradi huo ni baadhi ya wakazi ambao hawajalipwa fidia kukataa kuondoka eneo la mradi.
Mwananchi.   
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment