Meneja
Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji
litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni
hiyo, Daniel Wadelanga. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya
Nuebrand EC.
Mjumbe
wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba United Bank for Africa, Tesha Filemon
(katikati), akizungumza katika mkutano huo kuhusu kazi mbalimbali
zinazofanywa na benki hiyo.
Meneja
wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru
Idd (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo
na matawi yake.
Ofisa
Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani
(kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana
na na benki hiyo.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
Msimamizi
wa Masoko wa Kampuni ya Avic Town, Daniel Kure (kulia), akielezea kadhi
kadhaa zinazofanywa na kampuni hiyo katika mkutano huo. Kushoto ni
maofisa wa kampuni hiyo.
Meneja
Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Covenant Bank, Mhina Semwenda
(kulia), akizungumzia shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kifedha wakiwa
kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakiwa kazini. “Chezea kazi wewe”
Mmoja wa wanufaika na makongamano hayo yanayotolewa na Kampuni hiyo ya Nuebrand EC, Alphonce Mkubwa kutoka Mbeya akieleza faida ya makongamano hayo aliyoshiriki kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
……………………………………..
Na Dotto Mwaibale
TAFITI
zinaonesha asilimia kubwa ya watu hawatumii njia zilizo rasmi za
kifedha kutokana na kukosa elimu ya masuala ya kifedha na uwekezaji.
Hayo
yamesemwa Dar es Salaam leo na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya
Nuebrand, Cathreen Bukuku wakati akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari kuhusu kongamano la
wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi
30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambalo
litahusisha watu wote, wawe wajasiriamali au si mjasiriamali una
biashara au huna na wawekezaji wote ambapo washiriki watatoa kiingilio
cha ada sh. 2000/- kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo ambapo watapata
cheti cha ushiriki,”alisema Bukuku.
Alisema
lengo la kongamano hilo ni kuweka uelewa katika masuala ya kifedha
kwani watanzania wengi wamekuwa hawatumii njia zilizosalama na rasmi za
kifedha katika uwekaji, akiba na kutengeneza mazingira kuhusiana na
huduma za kibenki pamoja na ujasiriamali.
Bukuku
alisema washiriki watapata elimu ya uelewa wa bima mbalimbali kama za
maisha, afya na bima ya mali, kupata elimu ya jinsi ya kuandaa
mchamganuo mzuri wa biashara, kujifunza ujuzi mbalimbali na kupata fursa
ya kushiriki katika shindano la kuandaa mchanganuo wa biashara ambapo
atashinda fedha itakayomsaidia kuanzisha au kuendeleza biashara yake.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa,
alisema lengo lao ni kutoa elimu ya bima za maisha kwa watanzania na
kujua haki zao pamoja na kujua fursa zilizopo huku mshiriki akipata
huduma myimgi kwa wakati mmoja.
Mshindi
wa kongamano hilo msimu uliopita, Alphonce Mkubwa aliwataka vijana
kujitokeza kushiriki ili wapate elimu ya kufanya biashara ili wapate
mafanikio,” Nilikuwa mshindi katika kutoa wazo la biashara ambapo
nilishinda zabuni ya ukusanyaji ushuru katika halmashauri ya Wilaya ya
Chunya…huu ni muda wa kufanya kazi kwani huu ni ukombozi kwa kutokukaa
kijiweni,”alisema Mkubwa.
0 comments :
Post a Comment