Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn
Mworia akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa semina
mbalimbali wanazozifanya kama wadhamini wakuu kwa waendesha badabado
wakati wa maadhimisho ya wiki ya Usalama barabaranijijini dar es Salaam
yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam,
kwa Udhamini wa Vodacom Tanzania,Kulia kwake ni Mwenyekiti wa waendesha
bodaboda Wilaya ya Kipolisi Buguruni Kanda ya Tabata, Ramia Mazwela.
Mgeni
rasmi wa Uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es
Salaam,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova ( watatu
kutoka kulia) akiwa ameambatana na Maofisa wa jeshi hilo kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa wiki ya nenda kwa Usalama ikidhaminiwa na
Vodacom Tanzania.
Ofisa
wa jeshi la polisi Usalama barabarani,Koplo Wilbert
Biamungu(kulia)akimwelezea Mgeni rasmi wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa
Usalama barabarani Mkoa wa Dar es Salaam,Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, Suleman Kova(kushoto) akimuonyesha ramani ya barabara
inavyopaswa kutumiwa na kwa uadilifu na madereva wanaotumia vyombo vya
moto wakati huu wa wiki ya nenda kwa Usalama barabarani mkoa wa Dar es
Salaam inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu
wa kituo Usalama barabarani Mkoa wa Kipolisi-Kinondoni jijini,Solomon
Mangamiro(kushoto)pamoja na Ofisa Usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni
CPL Iyobu Madege(katikati)wakimsikiliza jambo Mkuu wa kitengo cha
Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(kulia)wakati
wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar es
Salaam yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Baadhi
ya Maofisa wa Jeshi la Polisi la Usalama barabarani na Magereza wakiwa
katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoa wa Dar
es Salaam yanayoanza tarehe 24-28 na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
0 comments :
Post a Comment