Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe

……………………………………………………………..
MABONDIA Ibrahimu Class ‘King
Class Mawe’ na Ally Mulo watapima uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya
mpambano wao wa jumamosi utakaofanyika katika viwanja vya basketball
vilivyopo katika shule ya uhuru wasichana Kariakoo Dar es salaam
Akizungumzia mpambano
huo mratibu ambaye pia ni kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu
Mhamila ‘Super D’ amesema mabondia hao watapima uzito siku ya ijumaa saa
tatu asubuhi kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi Agosti 22
Mbali na mabondia hao mabondia
wengine watakao onyeshana kazi siku hiyo ni Kelvin Majiba atakaepambana
na Vicent Mbilinyi wakati Husein Pendeza akioneshana umwamba na Shomari
Mirundi na Raymond Mbwago atazidunda na Roger Masawe na mapambano
mengine mengi ya mabondia chipukizi
Mabondia hao watapima uzito
katika tawi la mashabiki wa Yanga bomba lililopo mtaa wa Ndanda Kariakoo
na mpambano wao kufanyika siku ya jumamosi kuanzia saa kumi, mwisho
kabisa utakuwa utakuwa ni mpambano wa saa kumi na mbili jioni kati ya
mabondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ na Ally Mulo mpambano huo
umepangwa kuanza mapema ili kila mtu afurahie ngumi hizo na kurudi
nyumbani mapema


0 comments :
Post a Comment