MIKOA 10 ya Tanzania bara,
Inatarajia kuombea amani na utulivu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia
kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mikoa hiyo itaiombea amani
Tanzania kupitia muziki wa Injili kupitia waimbaji mbalimbali wa ndani
na nje ya nchi.
Msama alisema awali kabla ya
mikoa hiyo kuombea amani uchaguzi Mkuu, Tamasha la kwanza lenye dhamira
hiyo litafanyika Oktoba 4 jijini Dar es Salaam.
“Tumeona kuna umuhimu
kuwashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kumuomba Mungu atuongoze
katika uchaguzi Mkuu ambao unatakiwa kuwa huru na haki, ili kufanikisha
hayo kwa ufanisi nyimbo za kumuomba na kumtukuza Mungu zitumike ili dua
na sala zisikike mbinguni,” alisema Msama.
Msama alisema Kamati yake bado
inaendelea na mchakato wa kufanikisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo
litaimarisha na kudumisha amani na utulivu ulioasisiwa na baba wa Taifa
Mwalim Julius Kambarage Nyerere.
Aidha Msama alisema tamasha
hilo litashirikisha waimbaji mbalimbali wakiwemo wa Tanzania na nje
ambao watasaidia kufikisha ujumbe huo kwa Mungu.
Msama alisema wananchi
wajiandae kupata neno la Mungu kupitia waimbaji wa nyimbo za Injili
ambao watafanikisha mungu kusikia wanachohitaji wananchi.


0 comments :
Post a Comment