
Wafuasi
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Vwawa wakiwa
wambeba juu Fanuel Mkisi mara baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza,
kura za Maoni kumpata mgombea Ubunge uliofanyijka jana katika kanisa la
Moravian Mjini Vwawa. (Picha na Kenneth Ngelesi)

Mshindi
wa nafasi ya kwanza uchaguzi wa marudio kura za maoni wa kumpata
mgombea atakaye peperusha bendera ya chma cha Demokrasia na Mendeleo
(Chadema) Jimbo la Vwawa Fanuel Mkisi akiwa juu ya gari huku akipunga
Mikono kwa wafuasi wa chama hicho jana mara baada ya kutangazwa mshindi
wa kwanza kwa kupata kura 111.
Na Kenneth Ngelesi, Mbozi
KADA
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Funuel Mkisi ameibuka
kidedea kwa mara nyingine katika marudio ya kura za maoni za kumpata
mgobea atakaye peperusha bendera ya chama hicho nafasi ya Ubunge jimbo
jipya la Vwawa.
Akitangaza
matokeo hayo katika Kanisa la Moraviana Mjini Vwawa msimamizi wa
Uchuguzi Joseph Fyume kutoka Songea alisema kuwa Mkisi ameibuka kidedea
baada ya kujikusanyia kura 111 kati ya kura 179 zilizopigwa.
Alisema
kuwa wapiag kura walikuwa 179 ambapo hakuna kura iliyo haribika na na
kwamba zoezi hilo limeenda vizuri licha ya kuwepo misuguano ya hapa na
pale ambayo wajimbe walikuwa wakionysha kutoamiana kwa kiasi fulani.
Uchaguzi
huo ulishirikisha makada 13 wa chama hicho ambapo nafasi ya pili ni
Abaram Msyete aliye ambulia kura 28 wakati nafasi tatu alienda kwa
Steven Mwamengo kura 19 wakati kura zingine wakigawana.
Wagombea
wengine ni Solomon Kibona,Babu Mwapashi,Gifrt Kalinga,Fadhili
Shombe,Gerald Silyumba,Nzenga Simbeye Furaha Mwazembe,Andrew
Bukuku,Dickson Kibona na Jonadhan Mwashilindi ambapo kati ya hao wangine
waliambulia sufuri.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa mshindi Mkisi alisema kuwa aanshukuru wajumbe
kuonysha imani kwake kwa mara nyingine kwani licha ya uchaguzi wa awali
kutoridhiwa na baadhi ya wagombea lakini bado ameshinda nafasi hiyo kwa
kishindo.
Alisema
kuwa amekuwa akifanya saiasa kwa muda mrefu anaamani kuwa anauwezo ya
kunyakua jimbo hilo kwa kushikirikiana na wanachadema wote huku
akiwapongeza kamati kuu taifa kukubali uchaguzi huo urudiwe kwani
umekata mzizi wa fitina na kuondoa manung’uniko ambaye yangeweza
kujitokeza.
Katika
uchaguzi wa awali ambao ulifanyika Julai 21 mwaka huu ambapo Msyete
alijiondoka katikati ya mchakato kutokana na kutoridhishwa za hali
ilivyo kuwa siku hiyo na kulamika kukata rufaa,Mkisi aliongoza kwa
kupata kura 136 akifatiwa Mwamengo kura 42 na nafasi ya tatu alikuwa
Jonadhani Kinona ambaye aliambulia kura 22 tu.


0 comments :
Post a Comment