
Maofisa
wa Serikali kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali
wakiwa kwenye foleni ya kupima afya zao kwenye banda la Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya katika Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Serikali Mtandao mjini
Arusha.


Na Grace Michael, Arusha
MFUKO
wa Taifa wa Bima ya Afya umeombwa kutekeleza zoezi la upimaji wa afya
za wananchi katika Halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na utoaji wa
elimu ya namna ya kuepukana na magonjwa hayo ili kuliwezesha Taifa kuwa
na wananchi wenye afya imara.
Rai
hiyo imetolewa na watumishi mbalimbali katika mkutano wa kwanza wa
mwaka wa Serikali Mtandao uliofanyika mkoani hapa ambapo Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya ulitoa huduma za upimaji afya bure katika magonjwa
yasiyoambukiza.
Akizungumzia
hilo, Godfrey Luguma kutoka Halmashauri ya Wilaya Munduli alisema kuwa
ni vyema NHIF ikawa na ratiba ya kuzunguka katika maeneo yote ili fursa
hii iwafikie Watanzania wote.
“Upimaji
na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mifuko hii ikiwemo ya Afya ya
Jamii iendelee ili kila mwananchi aweze kutambua hali ya afya yake hatua
itakayomuwezesha kuwa na mipango imara ya kimaendeleo,” alisema Bw.
Luguma.
Naye
Nkide Mwaikuka kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa alitoa mwito kwa
wananchi kuhakikisha wanajiunga na utaratibu wa bima ya afya ili wawe na
uhakika wa kupata matibabu wakati wote.
“Bima
ya Afya ni mpango mzuri sana kwa watumishi wa umma na hata wananchi wa
kawaida, hivyo NHIF ongezeni elimu kwa wananchi hususan vijijini ili
watambue umuhimu wa kuwa au kutumia mpango huu,” alisema Bw. Mwaikuka.
Aidha washiriki wengine wametumia fursa hiyo kupima afya zao huku
wakiupongeza Mfuko kwa kuanzisha zoezi hilo kwa lengo la kuhakikisha
afya za watanzania zinabaki kuwa bora.
Akizungumzia
rai iliyotolewa ya upimaji ndani ya halmashauri zote, Mkurugenzi wa
Mifumo Habari wa NHIF, Othman Ali alisema kuwa mpango huo unafanyika
katika maeneo mengi ya nchi hii hivyo akawaomba wananchi kutumia fursa
hizo wakati zinapokuwa zimejitokeza.
“Tunazo
ofisi katika kila mkoa ambazo zinafanya haya majukumu kupitia mpango wa
Elimu ya Kata kwa Kata ambapo zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi
hufanyika,” alisema Bw. Othman.


0 comments :
Post a Comment