Mwaka huu
ni headlines za Uchaguzi 2015 tumeona baadhi ya wasanii wameonesha
kutoa support kwenye
kipindi hiki kwa wagombea Urais wawili ambao ni
John Pombe Magufuli atakaegombea CCM na Edward Lowassa kupitia CHADEMA.
Miongoni
mwa wasanii waliojitokeza na kutangaza rasmi kumsupport mgombea Urais
kupitia CCM, Dkt.John Pombe Magufuli, kuna Wema Sepetu, Batuli, Snura,
Linex, Steve Nyerere, Diamond Platnumz, Shetta, Barnaba,Bushoke, Kysher,
Wastara na wengineo huku mwigizaji Aunty Ezekiel na Jackline Wolper
wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni zamu ya Nay wa Mitego.
Nay wa
Mitego anamsupport Edward Lowassa kayaandika
haya....>>>>Huwezi zuia Mvua ikiamua kunyesha inanyesha tu!
Tuna Imani na Lowassa. Ccm wote bado wana Imani na Lowassa hata Kura za
Urais ni kwa Lowassa.Nilikua sipost chochote coz Nilikua nataka nisikie
CCM labda wana jipya juu ya sera yao mwaka huu coz upinzani umekua
mkali, wangenishawishi kidogo. Dooh ndo wameongeza uozo mara
dufu.Watanzania wameamka si kwa uongo ule wa jana Milioni Hamsini kila
Kijiji. Tanzania ina vijiji vingapi? Piga Hesabu ya haraka kadilia, si
chini ya bilioni 600 na zaidi.Watanzania sio mazoba kiasi hicho
tumeshtuaa...Hamjajipanga mwaka huu mmetukosa..#Mabadiliko2015
0 comments :
Post a Comment