WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akichukua fomu za
kuwania ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini kwa Msimamizi wa
Uchaguzi wa Wilaya ya Singida, Faridda Mwasumilwe katika Ofisi za
Halmashauri ya wilaya hiyo, juzi.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akipokewa kwa shangwe na wananchi
wa Kata ya Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini wakati
alipokwenda kuzungumza nao, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu na
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akicheza na makada wenzake wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kijiji cha Kinyagigi muda mfupi baada
ya kuchukua fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
WANANCHI wa Kijiji cha Kinyagigi katika Jimbo la Singida Kaskazini,
wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya kuchukua
fomu na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Singida.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati), ambaye pia
ni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwa na viongozi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Singida, muda mfupi baada ya
kuchukua fomu kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye pia ni mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, akiwahutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kinyagigi, jimboni humo juzi.








0 comments :
Post a Comment