Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, (Anayeshughulikia masuala ya Utawala),
Profesa David Mfinanga, (Watatu kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (watatu kulia), wakati
akipokea msaada wa magodoro 118 yaliyotolea wan Mfuko huo kwenye hafla fupi
iliyofanyika chuon I hapo, Agosti 24, 2015. Magodoro hayo ni kwa ajili ya
wanafunzi walioathiriwa na mogto uliozuka kwenye bweni kitalu B kule hosteli za
Mabibo, Aprili mwaka huu 2015.
NA
K-VIS MEDIA
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, leo Agosti 24, 2015, umekipatia Chuo Kikuu Cha Dar es
Salaam, UDSM, magodoro 118 ili kusaidia huduma ya malazi kwa wanachuo
walioathirika kutokana na bweni lao kuungua moto kwenye hosteli ya chuo hicho
Mabibo jijini Dar es Salaam Aprili mwaka huu.
Akikabidhi
msaada huo kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, (Anayeshughulikia
masuala ya Utawala), Profesa David A. Mfinanga, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
PSPF, Abdul Njaidi, amesema, PSPF, iliguswa na ajali hiyo ya moto ambayo
iliyotokea kwenye bweni kitalu namba B
na kusababisha mamia ya wanachuo kupoteza mali zao.
“Kwa
kutambua kuwa wanachuo ni sehemu ya jamii ya Watanzania, na pia ni wanachama
watarajiwa wa Mfuko, tumeona tuchangia sehemu ya vifaa ili wanafunzi waweze
kurejean katika hali yao ya kawaida.” Alisema Njaidi.
Akitoa
shukrani zake, kwa niaba ya Chuo, Profesa Mfinanga aliishukuru PSPF, kwa msaada
huo ambao kwa hakika umesaidia pakubwa, kwani magodoro hayo yatapelekwa kwa
walengwa na hivyo kusaidia kuwapunguzia machungu waliyoyapata kutokana na
kuunguliwa vifaa vyao.
Kwa
mujibu wa viongozi wa Chuo hicho, jingo hilo lilikuwa ,linakaliwa na wanachuo
788, wakati linawaka moto.
Profesa
mfinanga (wapili kushoto), akitoa shukrani kwa niaba ya chuo mbele ya maafisa
wa PSPF, viongozi wa wanachuo na
wafanyakazi wa chuo hicho wakati wa hafla hiyo
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akizungumza na
baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, baada ya kukabidhi
msaada huo, Agosti 24, 2015
Paulina Mabuga, mfanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dar
es Salaa, (wapili kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo. Wakwanza kushoto ni
Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Denis Bashulula
Profesa
Mfinanga na Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa
serikali ya wanafunzi UDSM
Mfanyakazi
wa UDSM, akipita jirani na magodoro hayo
0 comments :
Post a Comment