Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya
Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya
Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa
ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko
kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji
wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa
na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya
kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha
ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka
2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika
hoteli ya Ngurdoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo
pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha
ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka
2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa
Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika
warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya
Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa
iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi
yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya
uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014
iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa
mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa
umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa
zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu
Tawala wa Mikoa jijini Arusha.
Pichani juu na chini ni Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu
Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya
Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) katika picha ukumbusho na Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma, Chiku Galawa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani
Tabora, Queen Mlozi (kulia).
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa (kushoto) katika picha ya
ukumbusho na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema nje ya ukumbi wa
mikutano Ngurdoto Mountain Lodge.
Pichani juu na chini Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia
na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na
Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti
ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi
ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii
(ESRF), Dk. Tausi Kida akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mh. Hawa Ghasia mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI imesema itazingatia ushauri
uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya Mwaka
2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika warsha yao
iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa
Ghasia wakati akifungua warsha yenye lengo la kujadili na kuielewa.
Ripoti hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi
ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi
mwaka huu wa 2015 inawasilishwa kutokana na haja ya viongozi hao
kutambua yaliyomo na namna ya kusonga mbele katika mipango ya baadae.
Ripoti hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia
kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo ili kuwawezesha viongozi hao kupata
uelewa mpana juu ya dhana hii ya masuala ya Maendeleo ya Binadamu.
Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Ghasia alisema utafiti huo umelenga
kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na serikali za mitaa ili kuziwezesha
kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ripoti hiyo ambayo imezungumzia masuala ya
mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu imetafakari kwa undani
namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika taifa ili kuleta maendeleo
ya Binadamu.
Akizungumzia maendeleo alisema mwanzoni mwa
karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika yalitengeneza Dira za Maendeleo
kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na maendeleo.
“Kwa upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo
ya mwaka 2025 inalenga katika kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi
wa kati wenye kutegemea zaidi sekta ya viwanda na huduma.
“ Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya
Taifa 2025 inalenga siyo tu katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha
muundo wa uchumi; kwa miaka mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa
unategemea zaidi kilimo ambacho kina tija ndogo.” alisema Ghasia.
Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.
“Kwa mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967,
ambalo liliamua taifa lifuate mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza
kwamba sera, mipango na mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa
maisha ya watu kwani lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt.
Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba utafiti huyo
uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa kushirikiana na Wizara ya
Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na
ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar.
Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa yaliyopo hapa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP), Alvaro Rodriguez, alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya
kiuchumi ili taifa liwe la kipato cha kati.
Alisema ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha
kwamba linatumia vyanzo vyake vya kifedha kubadilika kutokana na hali
halisi ilivyo kwa sasa.
Aidha alisema ipo haja ya kuzingatia
mipango madhubuti ya kuondoa umaskini na kulinda mazingira, mambo ambayo
yapo katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo
kuanzia mwaka kesho hadi 2021.


0 comments :
Post a Comment