Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael..
Barnabas Lukindo akifanyiwa make up..
Husna Tandika akimpaka Natasha Mohammed model make up
Calorine-Benard. akifanyiwa make up
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania
katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa
na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show,
linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi
Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa
THT, Msami.
Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul
anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na
wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo
hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.
"Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu
katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu
zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming
Desgners'.
Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili
la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia
'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa
jina la Sanaa.".
Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki
kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo
nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.
Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.


0 comments :
Post a Comment