Mkufunzi na Mwandishi Mkongwe wa
Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim akitoa mada katika mafunzo
ya siku tano juu ya kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa
na Shirika la Habari la Marekani Internews kwa waandishi wa Habari wa
Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini
Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mhadhiri wa Sheria, Kitivo cha
Sheria Zanzibar University, Ali Uki akionyesha kitabu cha Sheria cha
Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kitabu cha Sheria cha Tanzania na
cha Zanzibar ambavyo vinawapasa waandishi wa habari kuvisoma na
kuzitumia sheria hizo katika kuandika habari za Uchaguzi Mkuu kwa
usahihi.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la
Zanzibar Leo Hafsa Golo akiwasilisha mada ya grop lake katika mafunzo ya
kuandika Habari za Uchaguzi Mkuu yaliyoandaliwa na Shirika la Habari la
Ineternews la Marekani katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu
Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Afisa Mwandamizi Baraza la Habari
Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan akiwasilisha mada ya
wajibu wa vyombo vya habari katika kuripoti Uchaguzi Mkuu katika mafunzo
ya waandishi wa Habari yanayofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye
ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar
Baadhi ya waandishi wa habari
walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi kutoka vyombo
mbali mbali vya Serikali na binafasi wakifuatilia mada zilizokuwa
zikiwakilishwa.
Mtayarishaji na Mtangazaji wa
vipindi wa Redio Zenj FM Mustapha Mussa akitoa mchango katika mafunzo
hayo yanayofanyika Ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Zanzibar.
Washiriki wa mafunzo ya kuripoti Uchaguzi Mkuu wakiwa katika kazi za vikundi wakijadiliana katika kufanikisha mafunzo hayo
0 comments :
Post a Comment