Kaimu Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye
aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa kambi hiyo ya upasuaji Johansen
Bukweri akizungumza kwenye uzinduzi huo, alisema magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele yamekuwa yakiathiri sehemu kubwa ya jamii katika
mkoa wa Mtwara na kuleta mahangaiko mengi kwa wananchi ikiwemo ulemavu,
hali ambayo inapunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika ujenzi wa
Taifa na watoto kutoweza kuhudhuria vizuri katika masomo shuleni
Mratibu wa Taifa wa Mpango wa
kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira,
akielezea majukumu ya mpango huo wakati wa uzinduzi wa kambi ya
kuwafanyia upasuaji watu wenye tatizo la ugonjwa wa mabusha Manispaa na
Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara,iliyofanyika katika hospitali ya Mkoa
ya Ligula.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi
wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) na Mwenyekiti wa magonjwa yasiyopewa
kipaumbele Afrika Dkt. Mwele Malecela akitoa salamu kwenye uzinduzi wa
kambi hiyo, ambapo alisema Matende na mabusha ni magonjwa ambayo
yanatakiwa kutokomezwa ifikapo mwaka 2020 nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga
,wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibimayila, akipokea
mfano wa hundi toka kwa mwakilishi wa Stat Oil Naomi Makota (kulia) kwa
ajili ya upasuaji wa wagonjwa wapatao 100 wa Manispaa ya Mtwara.
Kaimu Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kambi ya kuwafanyia upasuaji watu wenye ugonjwa wa mabusha.
Dkt. Upendo Mwingira akiwafariji
wagonjwa waliokwishafanyiwa upasuaji wa mabusha katika hospitali ya mkoa
ya Ligula.Upasuaji huo ni wa siku 5.Mkoa wa Mtwara una takribani watu
wapatao 2,500 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mabusha.Kambi hii itafanyika
kwa watu waliojiandikisha na itatolewa bila ya malipo
0 comments :
Post a Comment