WANANCHI wa vijiji vya Ilole, kitumbuka, Ilambilole, Ikengeza,
Chamdindi na vingine vilivyopo Katika wilaya ya Kilolo na Ismani
mkoani Iringa wailalamikia serikali kwa kushindwa kutatua kero ya maji
iliyodumu kwa muda mrefu Katika maeneo hayo.
Wakizungumza
kwa huzuni mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa aliyefanya ziara ya kugagua
miradi ya maji Katika wilaya hizo Mh Amina Masenza wananchi hao walisema
kumekuwa na ubabaishaji wa kisiasa juu ya namna ya kupelekewa maji
jambo ambalo linawafanya waweze kutumia maji yasiyo salama kwa afya zao.
Wananchi
hao walisema kumekuwa na miradi ya maji mingi ambayo ilitajiwa
kuwanzishwa Katika wilaya zao lakini mpaka sasa hakuna utekerezaji
wowote juu ya kutatua kero hizo pamoja na kuwa na vyanzo vizuri vya
maji.
“mh
mkuu wa mkoa tumeahidiwa sana juu ya kuletewa maji safi huku vijijini
matokeo yake hakuna lililofanyika tumekuwa watu wa kudanganywa kabisa
hata tukiangalia umbali wakilipo chanzo cha maji hata wangesema tuchimbe
mitalo wenyewe tungechimba ila wanatudanganya na siasa zao hatuyajui
maji ya baridi toka tunazaliwa tunatumia maji ya chumvi tuoneeni huruma
jamani” walisema wananchi
Akijibu
kero za wananchi hao mkuu wa mkoa Amina Masenza alisema kumekuwa na
watumishi wa serikali ambao wamepelekwa kusomea utalamu huo lakini bado
hawafanyi kazi sawasawa na elimu zao ambapo ameahidi kulishughulikia
jimbo hilo pamoja na kusimamia miradi mipya iliyopo ili iweze
kuwanufaisha wananchi kwa kupata huduma hiyo kwa urahisi.
“nimesikia
kilio cha wananchi sitakubali haya yaenelee kutokea wakati kuwa watu
wanapelekwa kusoma na serikali halafu hafanyi inavyotakiwa tafadhari
nataka kuona kazi mnayo ifanya ili wananchi hawa waweze kupata maji kwa
wakati kulinga na elimu zenu haiwezekani wananchi wangu wakawa wanaumia
na nyie mpo hapa haitawezekana”alisema Masenza
Aidha
aliwaagiza watendaji wa halmashauri na wataalamu wa sekta ya maji
kufanya uchunguzi Katika maeneo ambayo yanalalamikiwa na wananchi ili
kubaini chanzo cha tatizo na kukiondoa ili kuruhusu upatikanaji wa
huduma hiyo ikiwa n sambamba na wafugaji wanaotumia maji ya mto
kunywesha mifungo yao swan a watumiaji wengine wa kawaida ili kulinda
usawa Katika matumizi ya maji.
“ninawaagiza
kuanzia leo nendeni kuchunguza nini tatizo nataka majibu kuanzia sasa
na mniambie tatizo ninini linalofanya wananchi hawa wasipate maji mradi
umefika na pia wanaelimishwa juu ya matumizi ya mita na wale
wanaonywesha mifugo kwa mito wanatakiwa kulipiwa maji kwa kadiri na
idadi ya mifugo aliyonayo”alisema masenza
Kwa
upande wake Injinia wa Maji na meneja mradi wa Maji vijijini Bw Endru
Kisaru alisema kwasasa wanaongeza nguvu ya udhibiti wa matumizi ya maji
kwa kufunga mita kwani kwa sasa Katika jimbo la ismani idadi ya
watumiaji inakaribia 15000 ambapo kila kaya inaweza kulipa kiasi cha sh
5000 kwa mwaka ambapo tayari Unit 267 zimefungwa Katika maeneo hayo
hivyo amewahakikishia wananchi kwa tatizo na kero hiyo ya maji
itamalizika kwa wakati muafaka
“tutajitahidi
kutengeneza miundombinu ya maji itakayo hakikisha tunawafikishia huduma
ya maji wananchi wengi zaidi nawaomba wananchi wawe na uvumilivu wakati
tunaendelea kutatua baadhi ya changamoto zilizopo”alisema kisaru.
0 comments :
Post a Comment