Vijana
kutoka Tanzania wakiawa katika picha ya pamoja na msanii kutoka
Marekani Ne-Yo wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu
lililofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
Msanii
wa bongo fleva, Ali Kiba akiwa na msichana wa kitanzania Patricia
Kajange wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu
lililofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
Msanii
wa bongo fleva Ali Kiba akiwa na msichana wa kitanzania Barbara Mawalla
wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika
hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya
Kampuni
ya Coca-Cola kwa mara nyingine tena kupitia kampeni yake ya ‘Sababu
Bilioni za Kuamini’, wiki hii iliwapeleka vijana watano wa Kitanzania
kwenda nchini Kenya kushudia onyesho la Coke Studio Africa msimu wa tatu
ambapo, msanii maarufu duniani wa miondoko ya R&B kutoka Marekani,
Ne-Yo, alitumbuiza pamoja na wasanii wengine kutoka barai Afrika.Wasanii
kutoka Afrika ambao waliungana na Ne-Yo katika onyesho hilo wametoka
katika mataifa matano. Wasanii hao ni Ali Kiba(Tanzania), Wangechi
(Kenya), Maurice Kirya (Uganda), Ice Prince (Nigeria) na Dama Do Bling
(Msumbiji).Onesho hilo ambao
lilikuwa na msisimko wa aina yake kutokana na uwepo wa Ne-Yo, si tu
lilivuta hisia za mashabiki waliokuwa wakishuhudia studioni hapo bali
pia mamilioni ya wapenda mziki barani Afrika hasa kutokana na ujio wa
nguli huyo wa R&B ambaye mziki wake una mvuto wa aina yake.Vijana
hao ambao ni Patricia Kajange, Anderson Dickson, Annalisa Kiango,
Barbara Mawalla pamoja na Hilda Steven walionekana kuvutiwa na onyesho
hilo na kumimina shukarni zao kwa Coca-Cola kwa kuwapa fursa hiyo ambayo
ama hakika wamethibitisha kujifunza mengi kutokana na ziara hiyo.“Yaani
sijui hata niseme nini, maana leo ni kama siamini kumuona Ne-Yo ‘live’,
nimepiga naye picha na kumuona akitumbuiza moja kwa moja jukwaani”,
alisema Barbara Mawalla, miongoni mwa vijana watano waliokwenda
kushuhudia onyesho hilo.Kwa upande
wake, Patricia Kajange alisema, “Nina furaha ambayo hata siwezi
kuilezea hapa nilipo, nimefurahi sana kumuona Ne-Yo pamoja na wasanii
wengine hawa kama Ali Kiba na Maurice Kirya, nimefurahi sana kwa kweli”.Hilda
pia hakuwa nyuma kuzungumzia furaha yake mara baada ya kupata fursa
hiyo, “Yaani nilikuwa nimechoka kutokana na safari lakini baada ya
kushudia hili onyesho na kumuona kwa mara ya kwanza Ne-Yo kwa macho
yangu mwenyewe, na uchovu wote ukaisha, ni kumbukumbu kubwa sana
kwangu”.Anderson kwa upande wake
alisema, “aisee furaha niliyonayo siwezi hata kuielezea kwa sababu ni
kama ndoto zimetimia sasa, kumuona Ne-Yo live? sio jambo la mchezo,
nawashukuru sana waliofanikisha suala hili”Annalisa
alisema, “nimefurahishwa sana na jinsi wasanii hawa walivyoimba kwa
sauti yenye mpangilio na manjonjo ya aina yake, wakiongozwa na Ne-yo,
hili ni jambo la kipekee sana kwangu, ni historia nyingine hii katika
maisha yangu”.Baada ya kumalizika
kwa onyesho hilo pia vijana hao walipata nafasi ya kukutana na Ali Kiba
na kuzungumza naye machache pamoja na kupiga picha ambapo, Ali Kiba
aliwaambia amefarijika sana kuwaona vijana kutoka Tanzania maana
walimfanya ajisikie yupo nyumbani.“Nimefurahi
sana kuwaona na nimefurahi pia kwa sapoti yenu, ninyi kama Watanzania
wenzangu, ningependa kusema kuwa ni muhimu kujituma katika kile
mnachokiamini ili mtimize malengo yenu kwa sababu juhudi ndio kila kitu,
ndio maana tunasema lazima uwe na sababu bilioni za kuamini”.Coke
Studio Afrika ni onyesho linalofanyika kila kwaka likiwa na lengo la
kuwakutanisha kwa pamoja wasanii mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo
ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile
kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na wakubwa ili kuwapa
changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji
vyao.Mwaka huu, onyesho hilo
limeenda bega kwa bega na kampeni ya “Sababu Bilioni za Kuamini” ambayo
inalenga kuwahimiza vijana wote kujiamini juu ya ndoto walizonazo na
kupambana ili kutimiza ndoto hizo.Katika
msimu huu wa tatu wa Coke Studio Afrika, ni wasanii kutoka mataifa
matano tu tu ndio wamechaguliwa kutumbuiza. Mataifa hayo ni Nigeria,
Msumbiji, Kenya, Uganda na Tanzania.
0 comments :
Post a Comment