Mwenyekiti
wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Luis Benedicto (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi
kuanzia kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho, Jonas Lubago na Katibu Mkuu wa TLB,
Emmanuel Simon
Na Dotto Mwaibale
CHAMA
cha Wasioona Tanzania (TLB), kimetishia kutompa kura mgombea urais au
mwanasiasa yeyote kupitia chama chochote cha siasa ambaye hajaandaa
mazingira wezeshi na rafiki kwa ajiri ya kundi hilo kupiga kura.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Luis Benedicto wakati
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu wasiona kutengwa katika mchakato mzima wa uchaguzi
kuanzia kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
"Ndugu
wanahabari kundi la sisi watu tusioona tumetengwa katika mchakato mzima
kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 wa kuchagua rais, wabunge na madiwani
kuanzia kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura" alisema
Benedicto.
Alisema
mambo ya msingi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mwaka huu
hayajatazamwa wala kuzungumziwa ama na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
au vyama vya siasa nchini.
Alisema
zipo changamoto nyingi ambazo zinajidhihirisha hasa wakati huu wa
uchaguzi mkuu ambazo kwa vyovyote vile zinawanyima fursa na haki ya
kupiga kura kama watu wasiona ambao ni sehemu ya jamii.
Benedicto
alisema kwamba baadhi yao walihamasishana kadri walivyoweza
kujiandikisha katika daftari hilo ambapo walikumbana na changamoto
luluki.
Alitaja
baadhi ya changamoto walizokumbana nazo kutokana na kutokuona kwao ni
hawakutumia alama ya vidole gumba na badala yake walilazimishwa kushika
kalamu na kusaidiwa kuweka sahii kwa kusaidiwa na baadhi ya
waandikishaji jambo ambalo litaathiri taarifa zao nyingine zilizo katika
mfumo waliouzoea wa dole gumba.
Alisema
kutokana na kutotendewa haki hiyo wao kama Chama cha Waioona Tanzania
(TLB) kwa kauli moja wanatamka hawatawapa kura zao wanasiasa ambao
hawajaandaa mazingira hayo wezeshi na rafiki kwa ajili ya wao kupiga
kura.
Alisema
wanamashaka makubwa kama vyama vya siasa nchini vimeweka katika ilani
zao sera au kanuni zinazoelekeza utekelezwaji wa maslahi yao yanayogusa
moja kwa moja na changamoto za kimaendeleo wanazokabiliana nazo watu
wasiona.
Aliongeza
kuwa watu wasiona wana haki ya kushiriki na kuwepo katika vyombo vya
maamuzi ndio maana wanaviuliza vyama vya siasa kwamba vina mpango gani
wa kuwawezesha katika kushiriki katika majukwaa ya siasa katika kipindi
hiki na siku za usoni.
"Tunasikitika
kuona hata kanuni ndogo hazijatungwa ili kuwashirikisha watu wasioona
katika mchakato, jambo ambalo linatengeneza mazingira ya unyanyapaa
ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama kubwa za uchaguzi ambazo
walemavu wengi hawazimudu.
Alisema
kuwa elimu ya uraia, vifaa vya kupigia kura na miundombinu wezeshi
kufika vilipo vituo vya kupigia kura ni vitendawili ambavyo mpaka sasa
bado havijapatiwa hivyo kujiona wapo njia panda na hawajui itakuweje.
0 comments :
Post a Comment