Kulia ni mwanafunzi ambaye
alimtoroka mume wake baada ya baba yake mzazi kuamua kumozesha kwa
mahali ya ng’ombe 150 kushoto ni mama mlezi Veronica Kilango wakiwa
katika picha ya pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe
pamoja na maafisa kutoka shirika la Plan International mara baada ya
kumalizika kwa
mkutano na waandishi wa habari.
…………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZAZI na walezi hapa nchini
wametakiwa kuachana na mila zilizopitwa na wakati kwa kuwaozesha watoto
wao mapema hususan wa kike wakiwa katika umri mdogo na kupelekea baadhi
yao kukatisha masomo yao na badala yake wawe na mawazo chanya ya
kuwasaidia katika kuwalinda na kuwapatia haki zao za msingi katika
elimu.
Kauli hiyo imetolewa na
mwanafunzi mmoja anayesoma kwa sasa kidato cha tatu ambaye jina lake
linahifadhiwa kutokana na kulinda haki za watoto wakati wa ziara ya siku
mbili Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani iliyofanywa na shirikika la
kimaendeleo linalojishughulisha na kutoa misaada kwa binadamu Plan
International kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili watoto.
Mwanafunzi huyo akizungumza kwa
majonzi na waandishi wa habari pamoja na watendaji wa halmashauri ya
Kisarawe pamoja na watumishi wa Plan international amesema kwamba
amesikiteshwa sana kuona wazazi wake wanamkatisha masomo yake na
kumwozesha kwa nguvu bila lidhaa yake kwa mwanaume.
Aidha binti huyo amebainisha
kuwa baada ya mwaka 2014 mwanzoni kumkatalia baba yake mzazi kuolewa
ndipo mazi wake alipoamua kutumia njia nyingine ya kumdang’anya
anamtafutia uhamisho wa kwenda kusomea shule nyingine iliyopo Wilayani
Mkuranga kumbe alikuwa tayari amemtafutia mwanaume kwa nguvu kwa lengo
la kumwozesha mwanae.
Akielezea zaidi kuhusiana na
tukio hilo mwanafunzi huyo baada ya baba yake kumwozesha kwa mwanaume
huyo alikwenda kusihi nae kwa kipindi cha miezi miwli na baada ya hapo
aliweza kumtoroka na kukimbilia katika Wilaya ya Kisarawe ambapo
alimpata msamalia mwema ambaye anaishi nae kwa sasa.
“Kwa kweli mimi msichana mdogo
lakini kwa kitendo ambacho alinifanyia baba yangu kwa kuamua
kunilazimisha kuolewa kwa mabadilishano ya ng’ombe 150
nimesikitisikitika sana na mimi napenda sana masomo, hivyo wakati nipo
naishi na huyo mwanaume nilikutana na mtu mmoja nikwamwelezea akakubali
kunisaidia na ndipo nilipoamua kumtoroka na kwenda Kisarawe.”alisema
Mwanafunzi huyo kwa uchungu.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa
Jamii Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani amethibitisha kutokea kwa taarifa
za tukio hilo la mwanafunzi na kwamba wamempokea na kumpatia msaada wa
hali na mali ikiwemo kumpatia mahitaji muhimu na kumpeleka shule ambapo
kwa sasa anaendelea na masomo.
Kwa upande wake mmoja wa mjumbe
wa kamati ya ulinzi ya mtoto Wilaya ya Kisarawe Saimon Mpunga
akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake amesema kwamba kuja haja ya
kuwafichua wazazi wenye tabia kama hizo na kuongeza kuwa baada ya mradi
huo wa wa kupinga ukatili dhidi ya watoto kuanziashwa na Plan
International jamii imeweza kuvunja ukimya.
Mwandishi wa habari hizi
aliweza kupata fursa ya kuzungumza na mama mlezi ambaye anamlea
mwanafuzni huyo kwa sasa aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Kilango
ambaye alisema kwa sasa mwanafunzi huyo aliamua kumsaidia kwa hali na
mali na kwamba kwa sasa aneendelea na masomo yake katika shule moja ya
sekondari iliyopo wilayani Kisarawe.
Aidha Kilango alitoa wito kwa
jamii na wazazi kuhakikisha kwamba wanaachana na vitendo vya
unyanyasaji na ukatili kwa watoto wadogo na badala yake wabadilike na
kuhakikisha wanawalinda na kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo
kuwaendeleza kimasomo na sio kuwakatisha kwa kuwaozesha.
Naye Mratibu wa Mradi wa
kupinga ukatili kwa watoto kutoka Shirika la Plan International, Neema
Daniel alisema kwamba kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kunachangiwa
kwa kiasi kikubwa na jamii kutokuwa na mwamko mkubwa wa kutoa taarifa ya
kuwafichua watu wanaohusika na vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto
wadogo.
Kuanzishwa kwa Mradi huo wa
Plan International wa kupinga ukatili dhidi ya watoto umeweza kusaidia
kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kumpata na kumsaidia mwanafunzi huyo
ambaye aliozeshwa na baba yake mzazi kwa mwanaume mwenye umri wa mika
(30) kwa ng’ombe 150
0 comments :
Post a Comment