Chimbuko La Ugaidi ( 04)

  • Written @nkupama b
Ndugu zangu,
Jana ulimwengu umefikiwa na habari kuwa magaidi wamevamia hoteli ya Radisson Blu jijini Bamako, Mali na kuwateka nyara watu zaidi ya mia moja na hata kuwaua 27 miongoni mwao.
Al- Murabitun, ni kikundi cha ugaidi kilichothibitisha kuhusika na tukio la Bamako, Mali. Ibrahim Boubacar Keita, Rais wa Mali, yuko kwenye wakati mgumu kwa sasa katika kuongoza harakati za kupambana na hali iliyopo.

Hakika, ni habari nyingine ya kushtusha. Vikundi vya kigaidi aina ya Al- Murabitun ni tishio pia kwenye ukanda wetu. Ni katika wakati huu tuna lazima ya kutafakari harakati za kigaidi za kikundi cha Harakaat Al Shaabab
Mujaheedin , maarufu kama Al Shaabab. Al- Shaabab ni kikundi cha kigaidi kilicho nje ya ua wetu kama taifa. Kuna haja pia ya kuelewa ni nani wenye kuvifadhili vikundi kama hivi.
Mathalan, kuna taarifa za kiiintelijensia ambazo hazichambuliwi zikawekwa mezani. Hapa inahusu nafasi ya Ethiopia katika mgogoro wa Somalia uliozaa pia Al Shabaab.
Ni kuwa nafasi ya Ethiopia katika kuingilia kati na kupambana na Al Shabaab nchini Somalia imetokana na ukweli wa kihistoria, kuwa Ethiopia na Somalia kwenye miaka ya 70 wamekuwa kwenye mgogoro wa mipaka na hususan kwenye jimbo la Ogaden. Ni mgogoro uliopelekea vita pia.
Na ni Ethiopia iliyowahi kuingia Somalia na kupambana na Al Shaabab na hivyo kuvunja taratibu za utawala wa Sharia na uwepo wa Mahakama za Sharia. Ethiopia imekuwa mstari wa mbele katika kuisadia Serikali ya
Shirikisho ya Somalia. Ndio, Ethiopia ina maslahi ya moja kwa moja katika Somalia.
Hivyo basi, yumkini adui namba moja wa Al Shabaab ni Ethiopia na si Kenya. Na kwa kuangalia nadharia ya adui wa adui yako ni rafiki yako, tunaona uwepo wa mahusiano ya ajabu. Kwamba kuna taarifa ya uwepo wa mahusiano kati ya Eritrea na Al Shaabab. Maana, kwa miaka mingi aliyekuwa Rais wa Ethiopia, Merek Zenawi, alikuwa adui na Isaias Efeworki, Rais wa Eritrea. Hizi ni nchi jirani, na Marais wawili hawa inasemekana walikuwa na undugu pia. Huu ni uchambuzi endelevu...

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment