Dk Hellen Kijo-Bisimba Kupelekwa India kwa Matibabu

Saturday, November 14, 2015

  @nkupamah blog

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba anatarajia kusafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

Novemba 7, mwaka huu Dk Bisimba alipata ajali ya gari katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuvunjika mshipa wa paja na goti sanjari na kujeruhiwa kichwa,bega na mgongo.

Akizungumza jana akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Dk Bisimba alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anatarajiwa kupelekwa nchini humo na watoto wake kwa matibabu zaidi.

Alisema safari yake hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa huduma aliyoipata kutoka MOI bali ni kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi wa mwili wake.

“Namshukuru Mungu naendelea vizuri. Tangu nimekuja hapa MOI, nimesikilizwa na kuhudumiwa vizuri. Watoto wangu wanashugulikia usafiri na siku yoyote naenda India ,”alisema.

Meneja Uhusiano MOI, Jumaa Almasi alisema kuwa Dk Bisimba bado anahitaji uangalizi wa hali ya juu katika kipindi hiki kutokana na kupata majeraha mengi kwenye mwili wake.
 
 “Hali ya Dk Bisimba imevunja rekodi. Mbali na kumshughulikia sehemu hizo mbili (paja na goti), kutokana na kuwa na kisukari na presha tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment