Haya ndio maamuzi mapya ya mahakama kuhusu katibu mkuu wa zamani wa Simba

Friday, November 13, 2015

  @nkupamah blog

Baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miaka mitatu hatimaye Mwenyekiti wa Chama cha Soka Pwani (Corefa), Hassani Othman maarufu kama Hasanoo ameachiwa huru kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu.

Hasanoo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kusafirisha pembe za ndovu kutoka Dar es Salaam kwenda Hong Kong, zenye thamani ya Sh1.1 bilioni na wenzake amesota rumande kwa zaidi ya miaka miaka mitatu baada ya upande wa mashtaka kuizuia dhamana yake.

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba leo amemuachia huru Hasanoo na wenzake baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wanaominika, mmoja kati yao kuwasilisha fedha taslimu Sh 50 milioni ama hati ya mali yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Washtakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.

Hasanoo na wenzake wamekamilisha kasoro mmoja wao hakuwa na wadhamini hivyo amepelekwa rumande hadi atakapoyakamilisha masharti hayo.

Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka itaendelea kusikilizwa Novemba 17,2015.

Upande wa serikali iliwakilishwa na Mawakili, Paul Kadushi na Faraja Nchimbi.

Mbali na Hasanoo washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Ally Kimwaga, Dastan Mwanga, Godfrey Mwanga, John Mlai na Khalid Fazaldin.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Septemba Mosi na Novemba 20, mwaka 2012, kati ya Dar es Salaam na Hong Kong walikula njama ya kujihusisha na biashara ya nyara za serikali bila ya kuwa na leseni inayowaruhusu kufanya hivyo.

Kwa nia ovu walipanga, wakatekeleza, wakasimamia na kuwezesha kifedha kufanyika kwa biashara ya nyara za serikali kwa kusafirisha vipande 569 vya Pembe za ndovu, vyenye uzito wa kilogramu 1330 na thamani ya Sh 1,185,030,000 kwenda Hong Kong.

Siku hiyo ya tukio washtakiwa hao wanadaiwa kujihusisha na biashara ya nyara za serikali kinyume na kifungu cha 80 na 34 ya uhifadhi wa Wanyama Pori namba 5 na kwamba kwa nia ovu waliendesha biashara hiyo ya nyara za serikali bila ya kuwa na kibali halali kinachowaruhusu kufanya biashara hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment