Friday, November 13, 2015
@nkupamah blog
MCHAKATO
wa kujaza, kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Spikawa Bunge la Jamhuri
ya Muungano kwa wagombea ambao si wabunge, umemalizika rasmi jana
ambapo mgombea mmoja Profesa Costa Mahalu aliyewahi kuwa
Balozi wa Tanzania nchini Italia, alishindwa kurudisha.
Wagombea
waliorudisha fomu hizo ni Leonce Mulenda, Samuel Sitta, Gosbert
Blandes, Dkt. Kalokola Muzzamil, George Nangale, Banda Sanoko, Simon
Rubugu na Balozi Philip Marmo.
Wengine
ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Julius Pawatila, Dkt. Tulia Ackson, Mwakalila
Watson, Dkt. Didas Masaburi, Rita Mlaki, Veroikunda Urio, Chelestino
Mofuga, Agnes Makune na Abdullah Ali Mwinyi.
Job Ndugai achukua fomu
Aliyekuwa Naibu Spika katika Bunge lililoisha, Job Ndugai, jana alichukua fomu ya kuwania kiti hicho katika Ofisi ndogo za CCM, iliyopo Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Naibu Spika katika Bunge lililoisha, Job Ndugai, jana alichukua fomu ya kuwania kiti hicho katika Ofisi ndogo za CCM, iliyopo Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
baada ya kuchukua fomu, alisema rekodi yake ya kuongoza Bunge
inajulikana hivyo hana shaka na uzoefu wa kiti hicho na amewahi kuwa
Mwenyekiti wa Kamati za Bunge.
"Sina
wasiwasi kuhusu nafasi hii, Watanzania wanajuwa uwezo wangu wa
kuwatumikia hivyo naamini wabunge wezangu wateule wakinichagua
nitawatumikia kwa uweledi mkubwa," alisema.
Aliongeza
kuwa, amepata uzoefu wa kuongoza Bunge kupitia kwa Samuel Sitta, Anne
Makinda na akiwa mbunge tangu enzi ya Mzee Pius Msekwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa Bunge wakati huo.
"Najuwa
Bunge la 11 litakuwa na changamoto kubwa, kuna vijana wengi ambao ni
wapya lakini naamini nitawatumikia kwa kuwa Bunge linaongozwa na kanuni
hivyo nitazitumia kuwaongoza," alisema.
Amzungumzia Samuel Sitta
Ndugai alitumia fursa hiyo kumzungumzia Mzee Sitta akisema anatambua kuwa ni mwalimu wake lakini mwalimu hawezi kumzidi mwanafunzi hivyo hana shaka naye bali anaamini atachaguliwa.
Ndugai alitumia fursa hiyo kumzungumzia Mzee Sitta akisema anatambua kuwa ni mwalimu wake lakini mwalimu hawezi kumzidi mwanafunzi hivyo hana shaka naye bali anaamini atachaguliwa.
Rita Mlaki 'afunguka'
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Mlaki alisema amekaa bungeni miaka 10 kama mbunge na ameshika nafasi mbalimbali hivyo amepata uzoefu wa kutosha na anaweza kuitumikia nafasi hiyo.
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Mlaki alisema amekaa bungeni miaka 10 kama mbunge na ameshika nafasi mbalimbali hivyo amepata uzoefu wa kutosha na anaweza kuitumikia nafasi hiyo.
"Nataka
nafasi hii ili niweze kushirikiana na wabunge wenzangu kupitisha
Miswaada muhimu yenye maslahi kwa wananchi na kuweza kuisimamia,"
alisema.
Aliongeza
kuwa, lengo lingine la kuwania nafasi hiyo ni kuhakikisha anasimamia
suala zima la bajeti ya nchi na kuisukuma Serikali iweze kukusanya
mapato yake ya ndani bila kuwategemea wahisani.
Akizungumzia
nafasi ya mwanamke, alisema Bunge lililopita lilikuwa na Spika mwanamke
hivyo si tatizo kama ataingia tena mwanamke kutokana na uwezo walionao
sawa na wanaume.
Balozi Marmo arudisha fomu
Katika hatua nyingine, mgombea wa nafasi hiyo Balozi Philip Marmo, jana alirudisha fomu wa kuwania nafasi hiyo na kujivunia rekodi yake ya utumishi akidai ana uzoefu uliotukuka.
Katika hatua nyingine, mgombea wa nafasi hiyo Balozi Philip Marmo, jana alirudisha fomu wa kuwania nafasi hiyo na kujivunia rekodi yake ya utumishi akidai ana uzoefu uliotukuka.
Alisema
amesukumwa kugombea nafasi hiyo baada ya Rais Dkt. John Magufuli
kushinda nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25,
mwaka huu, kwani ni mtendaji mzuri ambaye anaamini atafanyakazi ya
kuijenga nchi ipige hatua ya maendeleo.
"Najua
Bunge la sasa litakuwa la kisasa kutokana kwa sbabu limejaa vijana
wengi lakini nawaahidi, nitaliongoza Bunge hilo kisasa zaidi na
kuwafanya wabunge watekeleze wajibu wao ipasavyo," alisema.
Dkt. Didas Masaburi naye arudisha fomu
Mgombea mwingine wa nafasi hiyo aliyerudisha fomu jana ni aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo, Dkt. Masaburi na kusema anafiti kuwa Spika kwani ana ubora unaozidi wagombea wote wa nafasi hiyo.

ana uzoefu wa kutosha kwani amewahi kuwa Mbunge wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki hivyo atahakikisha Bunge linaisimamia Serikali katika mikataba
mbalimbali kwa maslahi ya nchi.
Mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea ambao ni wabunge wateule unaisha Novemba 14, mwaka huu.
0 comments :
Post a Comment