KAMPUNI YA MSAMA PROMOTIONS YAMWAGA MISAADA VITUO 10 VYA YATIMA

t12Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
……………………………………………………………………………….
KAMPUNI
ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake,
Alex Msama, ilikabidhi misaada ya vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea
watoto yatima ikiwa ni
sehemu ya mapato ya matamasha yaliyopita.
Akikabidhi
misaada hiyo kwa watoto hao, Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua
nafasi yao katika jamii kwamba, watoto hao wanayo haki ya kupata
mahitaji muhimu katika makuzi kama wengine wenye wazazi wao.
Msama
alisema msaada huo wenye thamani ya sh. milioni 7.5, ni sehemu ya fedha
ambazo zimekuwa zikipatikana kupitia matamasha ya muziki wa Injili
ambayo ni wakati wa Pasaka na Krismasi.
“Msaada
huu ni sehemu ya fedha ambazo tumekuwa tukizipata kwa njia ya matamasha
ambayo tumekuwa tukifanya jijini Dar es Salaam na mikoani; Pasaka na
Krismasi,” alisema.
Msama,
alisema wamekuwa wakisaidia watoto yatima na makundi mengine maalumu
katika jamii kwa kutambua kuwa huo ni wajibu wa kila mmoja na ametoa
wito kwa wengine kuwa na moyo wa kusaidia makundi hayo.
Vituo
vilivyopata misaada hiyo ni Umra, Zaidia, Hiari, Malaika, Maunga,
Mwandaliwa, Sifa, Honoratha, Chakuwama na Rahman vya jijini Dar es
Salaam.
Miongoni
mwa vitu vilivyokabidhiwa ni unga wa sembe, mchele, unga wa ngano,
sukari, sabuni, mafuta ya kupikia, mafuta ya kupaka, dawa za meno na
vinginevyo.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea misaada
hiyo ya kiutu, viongozi wa vituo hivyo walisema ni faraja kubwa kwao na
watoto hao wenye mahitaji maalumu.
Maombio
Jonas, mwakilishi wa Kituo cha Sifa Group Foundation cha Bunju, ametoa
shukrani kwa Msama kwa moyo wa kujitolea kusaidia watoto wenye mahitaji
na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano wa moyo huo wa upendo.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo cha Hiari cha Chang’ombe, Aminajat Klemia, alitoa
pongezi kwa Msama kutokana na misaada hiyo akisema ni faraja kubwa kwa
watoto hao ambao wanahitaji kuthaminiwa kama wengine.
Misaada
hiyo imetolewa wakati ambapo kampuni hiyo ipo katika maandalizi ya
Tamasha la Krimasi litakalofanyika Desemba 25 kwa ajili ya kuadhimisha
kuzaliwa kwa Yesu Kristo pia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijalia nchi
kuvuka salama katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment