Majambazi Wateka Magari Huku Wakiimba "Hapa Kazi Tu"

Friday, November 6, 2015

@nkupamah blog

Kundi la watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha mbalimbali kama mapanga na marungu, juzi waliteka magari katika kijiji  cha Igogo,Wilaya ya Igunga huku wakiimba ‘hapa kazi tu’.

Baadhi ya madereva waliokumbwa na dhahama hiyo, walidai kuwa baada ya kusimamishwa na majambazi hao waliwashambulia kwa marungu na bapa la panga huku wakiwaamrisha watoe fedha na simu za mkononi huku wakitamka kila wakati kauli mbiu iliyotumika kwenye kampeni ya ' hapa kazi tu '.

Mmoja wa madereva hao alisimulia na kusema alikumbana na mkasa huo usiku wakati akitokea hospitali ya rufaa kupeleka wagonjwa.

“Wakati wakitushambulia kwa mapanga , majambazi hao walikuwa wakisema ‘hapa kazi tu, toeni pesa na simu'” alisema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment