Friday, November 6, 2015
@nkupamah blog
Mke
wa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, Regina Lowassa, ameikataa nafasi ya
ubunge wa viti maalum aliyopewa na kamati Kuu ya chama hicho cha
upinzani.
Kwa mujibu taarifa wa kutoka familia ya Lowassa iliyotufikia,
Regina anaichukulia kwa heshima kubwa nafasi hiyo, lakini anaamini
ataweza kushughulikia matatizo ya akina mama na watoto akiwa nje ya
bunge.
"Naishukuru
kamati Kuu ya chama changu kwa heshima hii kubwa waliyonipa na
ninaithamini sana, lakini naamini nitaendeleza mapambano ya kuwaletea
akina mama mabadiliko kwa ufanisi zaidi nikiwa nje ya bunge," amesisitiza mke huyo wa waziri mkuu wa zamani katika taarifa hiyo.
0 comments :
Post a Comment