Dk Mfinanga akipokea msaada huo leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya
Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha akiishukuru Kampuni ya
Matangazo ya Ashton Media leo kwa kutoa msaada wa viti, vitanda na
machela kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH).
Viti vilivyotolewa na kampuni hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni
ya Matangazo ya Ashton Media akiwapatia maji wagonjwa waliolazwa kwenye
jengo la Sewahaji katika hospitali hiyo.
…………………………………..
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH), leo imepokea msaada wa viti vitano kwa ajili ya shughuli za
utoaji damu, vitanda vitano vya kuzalisha kina mama na machela tano za
kubebea wagonjwa mahututi.
Msaada huo umepokelewa na Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel
Aligaesha na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dk Juma
Mfinanga wa hospitali hiyo.
Akizungumza katika tukio hilo,
Aligaesha ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo kwa kuwa utasaidia
kutoa huduma bora kwa wagonjwa.
“Kampuni hii imetupatia msaada mkubwa kwani ni moja ya msaada tuliokuwa tunauhitaji sana,” amesema Aligaesha.
Naye Dk Mfinanga amesema machela
zilizotolewa zitasaidia kubeba wagonjwa mahututi na kuwapeleka kwenye
kitengo hicho kwa ajili ya kupatiwa huduma kwa wakati na kuokoa maisha
ya wagonjwa.
0 comments :
Post a Comment