30, November 2015
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga
akielezea mambo mbalimbali katika semina hiyo. kulia kwake ni afisa
kutoka DIGNITY, Bi. Brenda Van Den Bergh. (Picha zote na Mpiga picha wa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora).
Tume
ya haki za binadamu na utawala bora ikishirikiana na Taasisi ya haki za
binadamu kutoka Denmark (DIGNITY) wamefanya semina inayohusu haki za
binadamu kwa kutoa elimu kwa asasi mbalimbali kuhusu haki za binadamu.
Akizungumzia
semina hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora,
Bahame Nyanduga amesema wameshirikiana na DIGNITY ili kutoa elimu kuhusu
haki za binadamu na kuiambia serikali kuhusu umuhimu wa kuzingatia haki
za binadamu.
Amesema
kuna baadhi ya sheria za haki za binadamu zimekuwa hazitekelezwi na
serikali zaidi kupitia Jeshi la Polisi ambapo kunaonekana kuwepo na
uvunjwaji wa haki za binadamu na kupitia semina hiyo watapata kutambua
haki za wananchi na umuhimu wa kuzifuata.
“Tunafanya
semina kushirikiana na wenzetu kutoka Denmark tunataka kutoa elimu
kuhusu umuhimu wa haki za binadamu jambo hilo linajitokeza sana na
tunachofanya ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza kumaliza tatizo hilo
ndiyo tunatoa elimu kupitia wao ambao ndiyo wanatenda mambo hayo unaweza
kuwa rahisi kumaliza tatizo hilo,” amesema Nyanduga.
Aidha
ameitaka serikali kusaini mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu ili
kusaidia kubana watu ambao wamekuwa hawafati sheria zilizopo na kuyataja
maeneo ambayo yamekuwa kunatokea vitendo hivyo kuwa ni pamoja na
magerezani na vituo vya polisi ili wakisaini vitendo hivyo vitaisha.
Kwa
upande wa Mkuu wa DIGNITY, Brenda Van Den Bergh amesema taasisi yao
imekuwa ikipambana kutetea haki za binadamu na wameamua kushirikiana na
watu wa haki za binadamu Ili kuongeza nguvu kuoambana na vitendo hivyo
na kuiomba serikali kusimamia haki za binadamu na kuwachukulia hatua
wale wote wanaovunja haki za binadamu.
Mwakilishi
wa Jeshi la Polisi katika semina hiyo, Kamishna Mwandamizi wa Polisi,
Yusuph Itembo amesema jeshi hilo limekuwa likifanya vikao na semina
mbalimbali kwa askari wao kuhusu jinsi ya kufanya kazi zao bila kuvunja
haki za binadamu.
Amesema
kuna makosa yanajitokeza na kutumia fulsa hiyo kuwataka Polisi wote
kufanya kazi kwa kufata sheria za nchi kama jinsi wanavyofundishwa
wakati wa mafunzo.
Mmoja
wa maafisa kutoka taasisi ya DIGNITY akitoa elimu ya masuala ya haki
za binadamu katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam makao makuu
ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Baadhi ya wadau katika seminaa hiyo..
Semina hiyo ikiendelea..
Mkutano huo ukiendelea…
Maafisa
wa tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini wakiwa katika picha
ya pamoja na Taasisi ya haki za binadamu kutoka Denmark (DIGNITY).
0 comments :
Post a Comment