Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa
kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya
miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani
yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu
Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiwa na baadhi ya viongozi wa kanisa
la Africa Inland Church wakati alipohitimisha maadhimisho ya miaka 20
tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi ya Pwani yaliyofanyika
kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere Kilwa
Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipohitimisha
maadhimisho ya miaka 20 ya Kanisa la Africa Inland Church Dayosi ya
Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa
Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim majaliwa akiwasha moja ya pikipiki tatu ili
kuashiria mkakati wa
kueneza injili wakati alipohitimisha maadhimisho
ya miaka 20 ya kanisa la Africa Inland Church Dayosisi ya Pwani kwenye
ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho wa Mwalimu Nyerere, Kilwa Road
jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akifurahia jambo na baadhi ya
viongozi wa kanisa la Africa Inland Church wakati alipohitimisha
maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo katika Dayosisi
ya Pwani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika uwanja wa maonyesho
wa Mwalimu Nyerere Kilwa Road jijini Dar es salaam Novemba 29, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………………………………….
*Asema Serikali hii siyo ya watu wapole
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim
Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kila
kinachokusanywa kama mapato ya nchi kinatumika kwa maslahi ya Watanzania
wote na si kwa manufaa ya wachache.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumapili, Novemba 29, 2015) wakati akifunga maadhimisho ya miaka 20 ya
Dayosisi ya Pwani ya Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT)
kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Serikali imeanza kukabiliana na
upotevu wa mapato ya Serikali na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ya
fedha za umma. Nia yetu ni kuhakikisha kila kinachopaswa kukusanywa kama
mapato ya nchi, kikusanywe na kitumike kwa masuala ya msingi kwa ustawi
wa Watanzania wote na si kwa watu wachache,” alisema.
Akifunga maadhimisho hayo kwa
niaba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Serikali
imedhamiria kupambana na maovu yote na kuondoa kero zinazowaumiza
wananchi wa kawaida. “Wako watu wanaoamini kwamba hatuwezi, nawaomba
waondoe hiyo dhana. Wako watu wanaodhani kwamba kwamba utawala huu ni wa
watu wapole, nao pia waondoe hiyo dhana,” alisema huku akishangiliwa na
mamia ya waumini waliohudhuria sherehe hizo zilizoanza Novemba 27,
2015.
“Tunawaomba Watanzania wote
mtuunge mkono kwenye vita hii na mtuwezeshe kuifanya kazi hiyo. Tunaomba
waumini wote mtuombee katika sala zenu za kila siku ili tuweze kuongoza
kwa haki na kuwaletea Watanzania wote maendeleo,” aliongeza.
Akinukuu kitabu cha Mithali sura
ya 29 mstari wa pili, Waziri Mkuu alisema: “Wenye haki wakiwa na amri,
watu hufurahi, bali mwovu atawalapo, watu huugua. Mtuombee viongozi wenu
tuwe waadilifu na wenye kutenda haki. Nasi tutaendelea kuwa waadilifu
ili watu wetu wasigue,” alisema.
Aliwataka viongozi wa kanisa hilo
waendelee kuisaidia Serikali katika kujenga kundi la watu wenye maadili
mema ili walisaidie Taifa kuwa na watu waadilifu na hivyo kupunguza kero
nyingi zinazoikabili jamii.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu
kuzungumza na waumini wa kanisa la hilo kutoka mikoa mbalimbali, Askofu
Mkuu wa Kanisa la AICT, Askofu Silas Kezakubi alisema Kanisa hilo
litaendelea kumuombea Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake ili wawe na
afya njema, wawe na hekima na kuahidi kwamba wataendelea kuwaweka chini
ya ulinzi wa Mungu siku zote.
Alisema wao kama kanisa wanaamini
kwamba Serikali ya awamu ya tano ina nia ya kuwatumikia wananchi kwa
bidii na uadilifu lakini akasisitiza kuwa siri ya bidii na uadilifu
inapatikana kwenye neno la Mungu.
Akisoma risala ya kanisa hilo,
Askofu wa AICT Dayosisi ya Kibaha, Askofu Charles Salalah alisema kanisa
halina budi kushirikiana na Serikali kwa sababu wote wanawahudumia watu
walewale isipokuwa katika malengo tofauti.
Alisema kanisa hilo linahubiri
maadili mema na bidii katika kazi kwa vile linaamini kuwa maendeleo
hayadondoki kutoka juu wala hayaoti kama uyoga bali yanapatikana kwa
watu kufanya kazi.
Akisisitiza kuhusu uadilifu,
aliwataka wazazi kudumisha ndoa zao ili watoto wapate malezi mema kutoka
kwa baba na mama na kwamba baba na mama wasipokaa vizuri, watoto
hawawezi kuwa waadilifu.
“Wazazi tunao wajibu wa kupanda
mbegu bora ya uzalendo kwa watoto wetu. Endapo tutapanda mbegu mbaya ya
kuwagawa watoto wetu kwa itikadi tofauti, ni lazima tujue kuwa tutavuna
tunachopanda.”
“Tukumbuke kuwa tunalo Taifa moja
tu la Tanzania. Hata kama watoto wetu watakuwa na upenzi na vyama vyao,
ni lazima tuwalee katika misingi ili wakue wakijua Taifa letu ni moja
tu. Ndiyo maana tunaweka mkazo kwenye familia kwa sababu maadili mema
yanaanzia nyumbani,” alisisitiza.


0 comments :
Post a Comment