KAGAME AMKATILI NKURUNZINZA HADHARANI



KIGALI,Rwanda

Rais PAUL KAGAME wa RWANDA amesema serikali yake haitapeleka askari wake kwenda kuungana na majeshi ya Umoja wan chi za AFRIKA yatakayokwenda kulinda amani katika nchi ya jirani ya
BURUNDI.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo huku akiendelea kupinga shutuma kuwa nchi yake imekuwa ikiwapatia silaha wakimbizi kutoka BURUNDI, ambao ni waasi.
Nchi HAMSINI na NNE wanachama wa Umoja wa AFRIKA, zinatarajia kupeleka askari Elfu tano nchini BURUNDI kwenda kulinda amani.
Hatua hiyo ni kuisaidia nchi ya BURUNDI isiingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Umoja huo unatarajia kupeleka askari wake nchini BURUNDI, licha ya upande wa upinzani nchini humo kudai kuwa hatua hiyo ni uvamizi wa mataifa ya kigeni.
Nchi ya BURUNDI ilijikuta katika ghasia, baada ya rais wan chi hiyo PIERRE NKURUNZIZA kutangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais kwa muhula wa tatu. Licha ya maandamano ya wananchi kupinga hatua hiyo NKURUNZINZA aligombea urais mwezi JULY mwaka huu na kupata tena fursa ya kuiongoza BURUNDI
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment