LONDON, England
Mchezo wa soka umeendelea kuwa
miongoni mwa mchezo unaopendwa na watu mbalimbali wa rika tofauti
tofauti katika maeneo tofauti tofauti duniani.
Lakini pamoja na hayo kazi kubwa ya
kuhakikisha mchezo huu unazidi kupendwa na
kuvutia machoni pa watu ni
pamoja na uwepo wa wachezaji mahiri,viwanja vya kisasa pamoja na
miundombinu ya uhakikka ya kufanya mchezo huo upendeze pindi
unapochezwa.
Lakini yote tisa kumi ni uwepo wa kocha
mzuri ambaye atatoa mbinu ambazo zitafanikisha uwepo wa mchezo
mzuri,lakini pia mbinu zitakazo mfanya mchezaji aonekane kuwa bora zaidi
pindi awapo dimbani.
Ifuatayo ni orodha ya makocha bora zaidi
katika soka la sasa ambao kutokana na mbinu zao wamezisaidia timu zao
kuweza kufanya vema na kucheza soka safi la kuvutia na ushindi.
KOCHA huyu aliajiriwa bila kutarajiwa, na hata msimu wa kwanza ulipomalizika kulikuwa na tetesi kwamba angefukuzwa kazi.
Lakini ametokea kuwa na mafanikio
makubwa kwenye msimu wa 2014/15 kwa kutwaa makombe matatu, ikiwa ni mara
moja tu kabla ya hapo walifanikiwa hivyo.
Kabla yake, Barca walifanikiwa kupata
vikombe vitatu msimu wa 2008/9 chini ya Pep Guardiola ambapo walitwaa
kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ubingwa wa La Liga na Kombe la Mfalme
au Copa Del Rey.
Chini yake, Copa Del Rey lilipatikana
baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Athletic Bilbao kwenye fainali
iliyofanyika nyumbani Camp Nou, wiki mbili baada ya kutwaa ubingwa wa
Liga kutokana na ushindi wa bao 1-0 nyumbani kwa Atletico Madrid,
Vicente Calderon.
Keki tamu zaidi ilifuata jijini Berlin
walipowasasambua Juventus kwa mabao 3-1 kwenye mechi ya fainali ya Ligi
ya Mabingwa Ulaya, kwa kupitia wachezaji Ivan Rakitic, Luis Suarez na
Neymar.
Huo ulikuwa ubingwa wao wa Ulaya wa mara ya tano, na Enrique ana kila sababu ya kuona fahari kwa mafanikio ya msimu huo.
Msimu huu pia umeanza vyema, ambapo
katika mechi tisa tu tayari walishajikusanyia pointi 21 wakitaka kutetea
ubingwa na kupambana na ushindani kutoka kwa mahasimu wao, Real Madrid.
2. Pep Guardiola (Bayern Munich)
Huyu ni kocha aliyetoka Barcelona, na
alifanya hivyo baada ya timu yake kufanya vibaya akaamua kukaa mwaka
mmoja akipumzika, kuibukia Allianz Arena.
Ikumbukwe kwamba ni msimu wa 2014/15 tu Bayern Munich walitwaa kombe kwa tofauti ya pointi 10.
Hata hivyo Guardiola aliiongoza klabu
yake kutolewa nje ya michuano ya Uefa Champions League ‘ UCL’ katika
hatua ya nusu fainali msimu uliopita, ambapo walitolewa na klabu yake ya
zamani ya Barcelona.
Kwenye Kombe la Ligi pia walitolewa kwenye hatua kama hiyo hiyo na Borussia Dortmund kupitia mikwaju ya penalti.
Msimu huu umeanza vyema wakitaka
kurekebisha makosa yao, wakiwa na nguvu ya mabao ya Robert Lewandowski.
Walishinda mechi zote 10 za kwanza, huku baadhi wakidai kwamba ubingwa
tayari nje nje.
Pamoja na hayo Guardiola anadaiwa kwamba
anaweza kuondoka mwisho wa msimu ili ajiunge na Manchester City kwa
ajili ya kwenda kuchukua nafsai ya kocha wa sasa wa timu hiyo Manuel
Pellegrini ambaye bado hajaushawishi uongozi wa klabu hiyo kwa kazi
anayoifanya katika timu hiyo.
Amewaweka vizuri pia katika mwelekeo wa kutwaa ubingwa wa Ulaya. Alipata kuwa kocha bora 2011.
Dunia ilisimama pale Paris Saint-Germain
(PSG) walipowafunga Chelsea na kuwaondosha kwenye Ligi ya Mabingwa
Ulaya (UCL) mwezi Machi mwaka huu, na watu walianza kuiona klabu hiyo
kama miongoni mwa timu kubwa
Kwa kifupi ni kwamba Blanc na kikosi
chake walizoa kila kitu msimu uliopita nyumbani, kwani walitwaa Trophee
des Championes (Super Cup) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Guingamp.
Lakini pia walitwaa Kombe la Ligi
walipowafunga Bastia 4-0, kisha Kombe la Ufaransa kwa kuwapiga Auxerre
1-0 katika fainali na kisha ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 kwa
tofauti ya pointi nane dhidi ya waliowafuatia Lyon.
Vijana wa Blanc pia wameanza vyema msimu
huu wakiwa moto chini na Zlatan Ibrahimovic wao wakienda vyema kwenye
Ligi Kuu na pia katika UCL.
5. Arsene Wenger (Arsenal)
Huyu anaitwa profesa wa soka
aliyewawezesha Arsenal kutwaa Kombe la FA mara mbili mfululizo na ndio
wanalishikilia bado, likiwa ni la pili kwa ukubwa England baada ya
ubingwa wa nchi.
Huyu ni kocha veterani kwani amekaa
Arsenal mwaka wa 19 sasa, akiongoza kwa kukaa katika klabu moja kwa muda
mrefu zaidi England, nchi yenye ligi maarufu zaidi.
Wenger (66) amejikusanyia kikosi chenye
mtindo wa aina yake, ubunifu na wachezaji wenye vipaji kama Sanchez,
Mesut Ozil na Santi Cazorla, na walitwaa Kombe la FA kwa kuwacharaza
Aston Villa 4-0 dimbani Wembley Mei mwaka huu.
Kwa jinsi Ligi Kuu ya England
inavyosonga mbele, kuna kila dalili kwamba Arsenal wanaweza kupanda na
si ajabu wakachukua ubingwa japokuwa wanaandamwa na majeruhi wengi.
Mmoja kati ya makocha wanaong’aa Ulaya
katika kizazi hiki ni Diego Simeone wa Atletico Madrid aliyewawezesha
kutwaa ubingwa wa La Liga katika msimu wa mwaka 2013/14 pamoja na
kutofanya vema katika msimu wa 2014/15 ambao walimaliza katika nafasi ya
tatu.
Walizidiwa nguvu na Barcelona na Real Madrid na msimu huu unaelekea
kuwa mgumu hivyo hivyo lakini raia huyu wa Argentina haoneshi dalili za
kukata tamaa, bali anakomaa na vigogo hao.
Amekuwa akikuza na kuendeleza vipaji
katika klabu hiyo yenye maskani yake katika dimba la Vicente Calderon
kwa miaka kadhaa sasa na amekuwa akiwindwa na klabu kadhaa, ikisemekana
kwamba hata Chelsea wanafikiria achukue nafasi ya Jose Mourinho.
7. Massimiliano Allegri (Juventus)
Mwanzoni mwa msimu wa 2014/15 ni
wachache walikuwa wanamuwazia au hata kumjua kocha huyu, lakini
alivyowaongoza Juventus kwa mafanikio, ikiwa ni pamoja na kufika fainali
za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha
miaka 12.
Klabu hiyo ilipatwa majanga ya kushushwa
daraja kutokana na kashfa ya Calciopoli ya kupanga matokeo na kutinga
Old Trafford 2003, Allegri aliwaongoza wachezaji wake kama Andrea Pirlo,
Arturo Vidal na Carlos Tevez kuwapiga timu kama Borussia Dortmund na
kwa makeke zaidi, Real Madrid kisha kwenye fainali dhidi ya Barcelona
jijini Berlin ambapo waliopoteza kwa kufungwa goli 3-1.
Kwa ujumla ulikuwa msimu mzuri kwa ‘bibi kizee cha Turin’ lakini Huenda
kupoteza wachezaji watatu niliowataja hapo huu ni moja ya sababu za
kuanza msimu wa 2015/16 bila kasi kubwa, wakiwa chini ya nusu ya jedwali
la msimamo wa ligi, lakini kuna dalili za kufyatuka na kupanda juu.
8. Jose Mourinho (Chelsea)
Pamoja na hivi majuzi tu kufutwa kazi ya
kuinoa Chelsea, alipata kudhaniwa kwamba angekuwa kocha bora kabisa
duniani, kutokana na mwelekeo wa mafanikio yake akiwa na Chelsea sasa
katika awamu ya pili.
Hata hivyo, ameanguka kwa kiasi kikubwa
kutokana na kuanza msimu vibaya kuliko alivyopata kufanya katika awamu
zake zote akipoteza mechi bila mpangilio na kuishia kutimuliwa na
uongozi wa klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu.
Lakini isisahaulike kwamba amefanikiwa kuzoa vikombe kadhaa na
kujenga jina kubwa la Chelsea katika awamu zake zote. Alitwaa Capital
One Cup kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham Hotspur dimbani Wembley,
lakini pia ubingwa wa England kwa tofauti ya pointi nane wakiwaacha
Manchester City nafasi ya pili.
Mourinho anajulikana kwa jinsi
anavyowapelekesha wachezaji wake, akiwapa mazoezi na kushikilia nidhamu
ambapo msimu wote uliopita walipoteza mechi tatu tu na hapakuwepo hata
moja waliyofungwa wakiwa nyumbani Stamford Bridge.
Mreno huyu mwenye umri wa miaka 52
amekuwa akitumia mbinu za aina yake, akichanganya ufundi, nguvu na haiba
yake kutisha wapinzani, hasa makocha kabla ya mechi hivyo kuwaathiri
wachezaji wa timu pinzani kisaikolojia.
Utawala wa Sevilla kwenye Ligi ya Europa
msimu uliopita ulikuwa wa aina yake, ambapo kocha Unai Emery aliwapa
ubingwa huo na kuwaingiza moja kwa moja kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
msimu huu, akiweka historia kwa mara ya kwanza katika mchakato huo.
Sevilla wametwaa ubingwa huo mara nne, nyingi kuliko timu nyingine
yoyote katika historia ya mashindano hayo, makombe mawili yakiwa chini
ya kocha huyo.
Walitwaa ubingwa msimu uliopita baada ya
kuwachapa Dnipro 3-2 kwenye fainali ya kuvutia iliyofanyika jijini
Warsaw, Poland, kwa mabao ya Carlos Bacca.
Hata hivyo, msimu huu Bacca ameondoka
pamoja na nyota wengine kadhaa, hivyo kufanya kuanza msimu kwa tabu
kidogo na kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo walikuwa na
kibarua kigumu mbele ya Juventus na Man City ambapo hata waliishia
katika nafasi ya tatu.
Hata hivyo, nyumbani wamefanya vyema,
ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya Barcelona. Bado yupo chini kidogo
akilinganishwa na majina mengine makubwa ya makocha hadi atakapopata
mafanikio mfululizo na timu yake.
10. Carlo Ancelotti (Real Madrid, alifukuzwa Mei)
Kutokana
na Real Madrid kumaliza katika nafasi ya pili kwenye La Liga msimu wa
2014/15, kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katika nusu fainali na
kuishia hatua ya 16 bora kwenye Copa Del Rey, kupoteza pia mechi ya
fainali ya Super Cup, Carlo Ancelotti alifukuzwa kazi.
Aliondoka Santiago Bernabeu Mei mwaka huu, lakini ukiwa ni mwaka mmoja tu tangu awapatie ubingwa wa Ulaya.
Kwa sasa Mtaliano huyo yupo benchi, hana
kazi kutokana na Real kutokuwa na subira. Alikuwa akihusishwa na
kujiunga Liverpool lakini nafasi hiyo imechukuliwa na Mjerumani Jurgen
Klopp.
Huenda hataajiriwa tena kufundisha timu
hadi msimu ujao, lakini amekuwa akihusishwa pia na Chelsea, kwani ni
kocha mzuri, mwenye umri unaofaa na amejikusanyia mafanikio mengi
yaliyotokan na kutwaa mataji yote makubwa Ulaya isipokuwa kombe la Euro
akiwa kama kocha.
0 comments :
Post a Comment