Lema atangazwa mshindi Jimbo la Arusha Mjini


  @nkupamah blog

Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura 68,848 kati ya
kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9 akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na asilimia 34.4.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na Navo Mollel wa ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy, jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment