MHAGAMA; Msiajili wataalam kutoka nje kwa kazi wanazoweza kufanya watanzania

x39
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akisisitiza kutoa kipaumbele cha ajira kwa
wataalam wa kitanzania wenye taaluma sawa na  wataalamu wasio watanzania wakati alipokutana na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za  Ajira Tanzania (TAESA),  tarehe 23 Desemba, 2015,  (katikati) ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Anthony Mavunde (Mb), na Kaimu Mkuu mtendaji wa Wakala wa Huduma za  Ajira Tanzania (TAESA), Boniface Chandaruba.
(Picha na Ofisi ya Waiziri Mkuu)
x40
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb) (wapili kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA), tarehe 23 Desemba, 2015,  wapili kutoka kushoto waliokaa),ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Anthony Mavunde (Mb).
………………………………………………………
Na. Mwandishi Maalum.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), amewaagiza waajiri wote nchini kutoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania wenye sifa za ajira ambazo ni sawa na zile walizonazo wataalamu wa kigeni kama sheria ya Kuratibu Huduma za Ajira kwa Wageni wa nchi za nje Na.1 ya mwaka 2015 inavyowaelekeza.
“ Sheria hii ya Kuratibu Huduma za ajira inatoa mwongozo ambao inawataka wale wote wanaokuja hapa nchini kwa minajili kutafuta ajira lazima wawe na kibali cha Kamishina wa Kazi wa hapa nchini, lakini pia Kamishina wa kazi ili atoe kibali hicho lazima ajiridhishe kuwa kibali anachotaka kutoa kama kweli hakuna mtanzania mwenye sifa na uwezo wa kufanya kazi husika na ndio sasa atoe kibali, tukizingatia haya tutakuwa tunatoa kipaumbele cha ajira kwa watanzania katika sekta mbalimbali” Amesema
Amesema hayo wakati akizungumza na Menejimenti ya Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA), alipokutana nayo Jijini Dar es Salaam, Desemba 23, akiwa ameambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Anthony Mavunde (Mb), kama sehemu ya kujifunza majukumu na kuelewa changamoto zinazozikabili Taasisi na Idara zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alibainisha kuwa kwa mwaka huu tayari watanzania wenye sifa za kuajirika 16000 wamejisajili kwa Wakala huyo na watanzania 8000 wameunganishwa na waajiri, lengo ikiwa ni kutoa kipaumbele kwa watanzania katika ajira hasa vijana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi.
Bibi Mhagama alisema: “Wakala wanalojukumu la kuwaunganisha watanzania na hasa vijana katika soko la ajira la ndani na nje ya nchi. Hivyo jukumu hili linawalazimu wafanye utafiti wakuelewa ni sehemu gani kuna nafasi za ajira kwa waliosoma elimu ya juu na wale wenye elimu ya kati, lakini pia na kuwasaidia watanzania hao wanaofika kwa Wakala huyo kuandaliwa ili waweze kuajirika” alisema
Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA) ilianzishwa kwa sheria ya Huduma za Ajira ya mwaka 2007 leno ikiwa ni kuwasaidia watanzania kupata kazi zenye staha na zenye mazingira rafiki kwa kazi husika ikiwa ni pamoja n akuhakikisha kuwa wanalipwa mishahara inayostahili kwa mujibu sheria za hapa nchini.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment