MUZIKI:Utanipenda ya Diamond yatazamwa na watu zaidi ya 800,000

Diamond

Video mpya ya staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz imetazamwa na watu zaidi ya laki nane
na tisini kwa muda wa wiki moja tangu itoke Desemba 11, mwaka huu.
Mkali huyo wa Bongo Fleva anatarajia kuangusha bonge moja la shoo ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar siku ya Krismasi, keshokutwa.
DIAMOND (3)  
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Akizungumzia maandalizi ya shoo hiyo, Diamond alisema itakuwa ya tofauti. Kila atakayelipia fedha yake ( kawaida shilingi 15,000 na V.I.P shilingi 30,000) hatojutia.
“Tukutane pale Dar Live, tuimbe na kucheza nyimbo zote za Diamond kuanzia Kamwambie, Lala Salama, Moyo Wangu, Mbagala, Nimpende Nani, Nitarejea, Ukimuona, Nataka Kulewa, Kesho, Nasema Nao, Mawazo, Number One, Nana, Nitampata Wapi, Kizaizai, MdogoMdogo, BamBam na Utanipenda ambao ndiyo habari ya mjini kwa sasa,” alisema Diamond.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment