Nkupamah media
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria
Rais wa
Nigeria, Mohammadu Buhari, ameiambia BBC kuwa majeshi yake yanakaribia
kulishinda kundi la kiislam , Boko Haram. Rais Buhari ameeleza kuwa
kundi hilo halina uwezo tena wa kufanya mashambulizi
dhidi ya majeshi ya
serikali ama maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na kwamba visa vya
kujitoa muhanga vimepungua .
Buhari
ameeleza kuwa kundi hilo awali lilikuwa na umoja ingawa kwa sasa
limesambaratishwa vibaya katika majimbo ya Adamawa na Yobe na kusalia
katika jimbo la Borno .
Boko
Haram wanaripotiwa kuendesha mashambulizi zaidi ya mia moja na kuua watu
zaidi ya elfu moja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita .
Ikumbukwe
kwamba ,wakati wa kampeni zake kuelekea uchaguzi nchini Nigeria,Rais
Buhari alitoa ahadi ya kupambana na kundi la Boko Haram mpaka kufikia
mwisho wa mwaka huu.BBC


0 comments :
Post a Comment