Kiongozi
wa waasi katika Jamhuri ya Afrika ya kati ambaye mwezi huu alitangaza
jimbo huru lililo chini ya uongozi wake, amesema ameacha kuupinga
uchaguzi muhimu unaofanyika mwishoni mwa juma hili nchini humo.
Noureddine
Adam, anayekiongoza kikundi cha FPRC kilichokuwa muungano wa waasi wa
Seleka ametajwa kama "Adui nambari moja" na serikali ambayo ilikuwa
imeitisha kukamatwa kwake kufuatia jaribio lake la kupinga kufanyika kwa
uchaguzi.
Tangazo
hili limejiri baada ya mazungumzo ya siku kadhaa yaliofanyika katika
nchi jirani ya Chad yaliyonuiwa kuondoa kikwazo kitakachokwamisha
uchaguzi wa rais na bunge siku ya jumapili, uchaguzi unaoangaliwa kuwa
muhimu katika kumaliza miaka kadhaa ya umwagikaji damu.
"Vuguvugu
letu linaahidi kutoa mchango chanya na wa kweli ili uchaguzi ufanyike
kwa utulivu, bila vurugu na utakaowashirikisha raia wengi," ilisema
taarifa iliyotolewa na utawala wa Chad ulioshiriki mazungumzo hayo.
Noureddine
Adam, alikuwa kamanda wa pili katika kundi la waasi wa kiislamu wa
Seleka lililochukua madaraka mwanzoni mwa mwaka 2013 katika taifa hilo
lililo na wakristo wengi, na kumuondoa madarakani rais wa wakati huo
Francois Bozize.
Kampeni za uchaguzi zaanza
Kampeni
za uchaguzi zilianza hapo jana huku wagombea wasiozidi 30 wakitarajiwa
kugombea nafasi ya urais. Aidha Bozize, aliyeishi uhamishoni hasa nchini
Uganda tangu alipotolewa madarakani, alinyimwa nafasi ya kugombea
katika uchaguzi wa jumapili baada ya mahakama ya kikatiba kukataa ombi
lake mapema mwezi huu.(P.T)
Kando na
hilo bado Bozize anaungwa mkono na raia wengi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati hasa katika eneo la Kusini Magharibi, siku ya Jumanne chama chake
cha
Kwa Na
Kwa (KNK) kilimuunga mkono mgombea aliye na miaka 58 Anicet-Georges
Dologuele, hatua inayoonekana huenda ikatoa nafasi ya ushindi kwa
mgombea huyo aliyekuwa Waziri Mkuu nchini humo.
Awali
katibu Mkuu wa chama hicho cha KNK Bertin Bea alimwambia mgombea
Anicet-Georges kwamba watafanya kila wawezalo kuhakikisha anashinda
katika duru ya kwanza ya uchaguzi, na kumhakikishia kuwa ana uungwaji
mkono mkubwa kutoka kwa chama hicho, wanaharakati na hata Francois
Bozize."
Mgombea
mwengine katika uchaguzi huo ni Martin Ziguele, anayesemekana kupata
uungwaji mkono kutoka koloni la zamani la nchi hiyo Ufaransa.
Wagombea
wengine wanaoonekana kuwa na nafasi ya kuchukua ushindi ni Karim
Meckassoua, na Xavier Sylvestre Yangongo, jenerali wa zamani ambaye
mabango yake ya kampeni yanamtaja kama nguzo ya Jamhuri ya Afrika ya
Kati. Iwapo hakutakuwa na mshindi wa moja kwa moja siku ya jumapili duru
ya pili ya uchaguzi itafanyika tarehe 16 mwezi wa Januari.
Uchaguzi
nchini humo umecheleweshwa kwa muda mrefu, kura ya maoni ambayo ni hatua
ya kwanza ya kupisha uchaguzi wa rais na bunge kufanyika ili kuirejesha
nchi katika utawala wa kidemokrasia kufuatia serikali mbili za mpito
ilifanyika mnamo tarehe 13 mwezi huu wa Desemba.
Chanzo:DW


0 comments :
Post a Comment